Bukobawadau

MAZISHI YA MAREHEMU MTENSA LEONARD NI KUMBUKUMBU YA KIHISTORIA MKOANI KAGERA

Vijana wa  kikosi kazi maalum wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mtensa Leonard  kutoka ndani ya Nyumba  kuelekea Ukumbini kwa ajili ya Misa ya Mazishi iliyohudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka Nje na Ndani ya nchi.
 Front line yupo Rahym Kabyemela na Jamal Kalumuna.

 Vijana Smart wakiwa kwenye vazi  aina ya suti wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mtensa Leonard aliyefariki hivi karibuni kwa kifo cha ghafla ambapo mpaka sasa chanzo cha kifo  hicho bado hakijajulikana 
Wanatembea kwa mwendo wa pole pole wakati wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu  Mtensa Leonard.
 Mjane wa Marehemu Mtensa Leonard.
 Pichani Kushoto ni Mzee Rugaibura
 Pole sana Benna pole sana Mama Deo  pole kwako mama Prince.
 Pichani ni  watoto watatu kati yawatano wa kuzaliwa na Marehemu Mtensa Leonard.
 Mzee Rugaibura, Mzee Frank Theophi na Mzee Mchuruza wakiendelea na Misa ya mazishi. 
 Pichani Katikati anaonekana Mr. Karoli wa Mutukula, huyu ni mmoja wa wafanyabiashara maarufu kwa ukanda wetu waliotokea kupatapa mafanikio makubwa kupitia  mikononi mwa Marehemu Mtensa Leonard ambaye leo Jumamosi Nov 22,tunampumzisha katika makazi yake ya milele
 Bi Letty akiendelea na misa hii maalum kumuaga Mpambanaji, mzalendo Marehemu Mtensa
 Katika sintofahamu anaonekana Bi Anitha David Mtensa.
 Shughuli ya Misa ikiendelea,hapa kikubwa ni mpangilio wa shughuli nzima,heshima kubwa kwa mwili wa Marehemu sanjari na Wingi wa watu ni hali iliyoongeza mazishi hayo kuwa ya aina yake.
 Mr. Ben Kataruga na Mr Justuce Rugaibura wakiwa wametoka Jijini Dar es Salaam kushiriki  shughuli ya mazishi ya Rafiki yao , Kaka yao mpendwa Marehemu Mtensa Leonard
Sehemu ya Wanakwaya.
 Mzee Baganda na Mzee Nyerere waliokaa mstari wa mbele.
Umati mkubwa wa watu  wakiendelea kushiriki Misa ya shughuli ya Mazishi ya Marehemu Mtensa Leonard nyumbani kwake Kyaikailabwa  takribani kilomita 3 nje kidogo ya Mji wa Bukoba
 Sehemu ya wanachama wapambanaji 'Wanapamoja' wakiendelea kushiriki  Misa ya kumuaga  Ndugu yao, rafiki yao ,kaka yao mpendwa na  mwanachama mwenzao mtu wa watu Marehemu Mtensa Leonard.
 Kutoka kushoto ni Mzee Baganda akifuatiwa na Mzee Philbart Nyerere na Mzee Pius Ngeze
 Mdau Yusuph Abed (Dj Y) na Ndugu Rahym (Dj Ray )hakika wameguswa sana na msiba huu.


Inasikitisha na kuhuzunisha ,pichani kushoto ni Mama Mzazi  wa Mjane wa Marehemu akiwa na  (Ma Kossi)ambaye ni Mama Mzazi wa Marehemu Mtensa kwa pamoja wanamlilia mpendwa wao
 Kutoka kushoto ni Jamal (Jamco)Kalumuna, Rahym Kabyemela, Mc Baraka (Bukobawadau), Ndg Rmk Ramadhani Maulid Kambuga Mr. Follo , Gilbart Gsmart George na  Ndg Samola Lyakurwa.
 Mr. Innocent Pajero , Mc Jerry na Ndugu Optaty Folo pichani.
 Kaka Mkubwa E.Nyambo anamwongoza Mama Mzazi wa Marehemu Leonard Mtensa kushuhudia.
 Bi Benna Kurji Mrs Deo ambaye ni shemeji ya Marehemu Leonard Mtensa
 Jeanifer Murungi KichwabutaWatoto wa Marehemu wakitoa heshima za mwisho..'Tutakukumbuka Baba yetu mpendwa'!
Watoto J mmoja wa marehemu wakiaga mwili wa baba yao huku wakilia kwa uchungu
Katika zoezi la kushuhudia anaonekana Mzee Yusto Mchuruza.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Ben Expeditions akitoa heshima za mwisho.
Mkubwa Justuce Rugaibura kutoka Jijini Dar es Salaam akitoa heshima zake za mwisho
 Mama Muhazi, rafiki wa familia akishiriki zoezi la kutoa heshima za mwisho
 Kaka Mkubwa Ernest Nyambo akitoa heshima za mwisho kwa rafiki yake,'katikilo wake' Mtensa
 Watu mbalimbali wakiendelea kuhushu
 Mh. Yusuph Ngaiza Diwani Kata Kashai mara baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake
 Mtawa wa kanisa Katoliki nchini akitoa heshima zake za mwisho kuuaga mwili wa Marehemu
 Mrs David Mtensa
 Sehemu ya Wafanyakazi wa Linas Club wakitoa heshima za mwisho
 Zoezi la kutoa heshima za mwisho likiendelea
 Mr.Minas Visram na Mr. Bandali wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa rafiki yao
 Waombelezaji wakiendelea kutoa  heshima za mwisho
 Hivi ndivyo hali ilivyokuwa ,ni hakika kifo cha Mtensa ni huzuni mkubwa
 Mzee Ojwambo katika zoezi la  kushuhudia.
Mzee Pius Ngeze  akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Marehemu
 The futuhi....
Shukrani za pekee kwako Bi Jeanifer Murungi Kichwabuta Bukobawadau tumeshuhudia namna  ulivyojitoa kwa nguvu zako zote kwa hali na mali  katika msiba huu .

 Mama Petel Mulima pichani
 Wadau wakiendelea kutoa heshima zao za mwisho kwa Mpambanaji Marehemu Mtensa.
 Mr. Deo Rugaibura, Uncle Salum na Ndg Optaty Kajuna (Follo)
 Mama Mwainunu akitoa neno na rambirambi kwa niaba ya 'Wanapamoja'
 Kaka Mkubwa Ernest Nyambo akitoa yake ya moyoni kwa niaba yake binafsi na kufikisha kile kilichotoka kwa Bukoba Veterans katika kusupport msiba huu mkubwa wa mwenzao.
 Waakirishi kutoka Kikundi cha Sanaa cha Futuhi wakiongozwa na Mdau Mzalendo Willy Kiroyera
Kutoka kundi maarufu la Futuhi la jijini Mwanza wameguswa sana na msiba huu 'Ebyehatari'!
 Mwalimu Bube, ambaye ndiye aliyekukuwa swahiba wa karibu na Marehemu anatoa utambulisho kwa watoto wa Marehemu kabla ya kusoma wasifu wake.
 Marehemu Mtensa Leonard ameacha Mjane na watoto wa tano,Wanne wa Kiume na Mmoja wa Kike, pichani ndiye  kitinda mimba kwa jina ni Stalon Mtensa.
Mr.Alfred Matovelo akiwa ametoka jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki mazishi ya rafiki yake
  Watu wanalia! wanahudhunika na machozi yanawatoka kufuatia msiba huu wa kihistoria.
Bi Linna Mtensa  mtoto mkubwa wa Marehemu Mtensa Leonard
 Katika Utayari kuubeba Mwili wa Marehemu Mtensa Leonard Kuelekea eneo la Kaburi
 Kuelekea eneo la Kaburi


 Wakati tukiendelea tunapokea Salaam za rambirambi kutoka kwa Ndg  Bennett Rweyemamu akiwa Dar es Salaam,anasema;'Nakumbuka mara ya mwisho kabisa miaka miwili nikiwa Bukoba Kaka Mtensa ndo alikuwa mtu wa mwisho kuachana naye, tumeachana karibuni saa saba usiku nikiwa na mdogo wake Mugisha na kesho yake nikapanda ndege kuelekea Dar es Salaam. Kwa kweli usiku ule nilifarijika sana sana kwa kuwa kwangu na Kaka Mtensa kwani tukiongea mengi sana na kanipa maneno makubwa sana kanizungusha kwenye miradi yake yooote na nikamuahidi tungeshirikiana pale ambapo tungeweza kuhitajiana'
 Kusema ukweli. Ni majonzi makubwa sana, sana kumpoteza mpiganaji mzalendo wa mkoa wa Kagera na mji wa Bukoba kwa ujumla. Kwa heshima zote nawatakia ndugu, familia, marafiki na jamaa wote moyo wa Subra kwa kupoteza JEMBE!!!!! Mungu akupokee Kaka Mtensa! Amen. (Bennett Rweyemamu-Dar es Salaam)
 Jeneza likiingizwa Kaburini
Mama Mjane akiweka Udongo kwenye Kaburi la mme wake Mpendwa.
 Mwalimu Jackson Buberwa akiweka Udongo kwenye kaburi
 Mama Mzazi wa Marehemu tayari kwa ajili ya kuweka shada la maua.
 Binti wa Marehemu Mtensa Leonard akiweka shada la maua
 Ndugu Optaty Kajuna anaweka shada la Maua.
 Utaratibu wa kuweka mashada ya maua ukiendelea.
Mr . Ben Kataruga na Mwenzake Justuce Rugaibura wakiweka shada la maua
 Kwa umahiri mkubwa Mr. Bube akielezea anavyomfahamu marehemu nje ndani anasema; Marehemu  Mtensa katika kuwepo kwake Duniani alipenda sana wimbo uitwao(I Will Always Love You wa Whitney Houston)hivyo anahakika wimbo huo ukipigwa mahali hapa tutakuwa tumetenda haki kwa Marehemu Mtensa Leonard


 Mr. Bube akiendelea kutolea jambo ufafanuzi
 Neno kutoka kwa Hajj Maulid Kambuga kwa niaba ya Wazee.
Sehemu ya waombolezaji
 Neno la Shukrani kwa wato walioshiriki shughuli ya kumuaga Mpendwa wetu linatolewa na Mwenyekiti wa kamati ya Mazishi Ndugu Self (Super) Mkude
 Mc Muongozaji akitoa utaratibu
 Anaitwa Linna, mtoto mkubwa au wa kwanza kuzaliwa na Marehemu Leonard Mtensa
Marabaada yashughuli nzima ya mazishi.
 Ndivyo linavyo onekana kaburi la Marehemu S.Leonard Mtensa likiwa na maua kila aina
 Mara baada ya Shughuli ya Mazishiwadau wakibadirishana mawazo
 Washirika wa Bukoba Veterans,Shukrani kubwa kwenu kwa niaba ya familia ya Marehemu
Mh.Rwaks  Wilfred Lwakatareameweza kushiriki katika maziko haya.
 Kikosi kazi maalum katika picha ya kumbukumbu
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Linas Night Club.
Rais wa COSAD Tanzani Ndg Smart Baitani
 Marehemu Mutensa alikuwa ni mpambanaji aliyejitahidi kuibadilisha Bukoba kwa jitihada za ujasitiamali. Ni miongoni mwa wazaliwa wa Bukoba ambao kwao Bukoba ilikuwa ni kila kitu, kuwekeza Bukoba kuna changamoto nyingi. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake litukuzwe. Tumuombe Mungu aipokee roho ya marehemu na ampatie pumziko la amani.
 Kwa matukio ya picha zaidi ya 200 unaweza  kujiunga nasi katika Ukurasa wetu wa facebook kupitia link hii hapa>> Bukobawadau Entertainment Media Next Post Previous Post
Bukobawadau