KITENDO cha Mkurugunzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba mkoani
Kagera, Joseph Mkude cha kuwafukuza waandishi wa habari na wananchi
katika vikao vya Baraza la Madiwani, kimelaaniwa na Mkuu wa wilaya hiyo
na madiwani.
Mkurugenzi huyo anadaiwa kukiuka kanuni ya kudumu namba 12 kifungu (1)
na cha (2) inayowaruhusu wananchi kuhudhuria vikao hivyo vya wazi.
Mdiwani hao ambao walitishia kususia na kuhairishwa kwa kikao cha
baraza cha Oktoba 31 mwaka huu, walimtaka mkurugenzi huyo, kurejea
matangazo yake aliyoyabandika katika mbao za matangazo za halmashauri
hiyo.
Tangazo hilo lilisomeka hivi; “Tangazo la mkutano wa Baraza la
Madiwani. Napenda kuwatangazia wananchi wote wa Wilaya ya Muleba kuwa
mkutano wa Baraza la Madiwani utafanyika tarehe 30/10/ hadi 31/10/2014,
kuanzia asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri”.
Kwa mujibu wa tangazo hilo lenye kumb. namba KGR/HW/ML/.A.33/Vol.X/19,
wananchi walikaribishwa kusikiliza kinachojadiliwa katika baraza hilo.
Hata hivyo, pamoja na tangazo lake hilo, Mkude aliingia ukumbini Okoba
30 mwaka huu, na kuwakuta wananchi pamoja na waandishi wa
habari waliokuwa wamehudhuria kikao hicho, watoke nje, jambo lilipingwa
vikali na madiwani.
Amri hiyo ya mkurugenzi, iliwafikisha waandishi kwa mkuu wa wilaya
hiyo, Lembris Kipuyo na kumweleza yaliyojiri ambapo aliwataka kuwa
wavumilivu wakati akiendelea kulishughulikia.
“Hata mimi sijapendezwa na kitendo hicho, kikao cha Baraza dogo ndio
chenye habari nyingi na nzuri zinazohusu wananchi, unajua mimi huwa
nawaambia viongozi wenzangu na watendaji wetu kuwa Muleba hii ina watu
zaidi ya laki tano, sasa leo tukitaka wananchi wajue serikali yao
imefanya mambo fulani lazima tutumie vyombo vya habari.
“Hata Rais Kikwete wakati tuko Dodoma katika semina elekezi mwaka
2006, alitueleza kuwa tukitaka mafanikio lazima tufanye kazi kwa karibu
na vyombo vya habari, leo mkurugenzi amejisahau, nitamuita
nimweleze,”alisema Kipuyo.
Alisema kuwa Muleba ikiharibikiwa pia naye ataharibikiwa kwa sababu
kikao hicho kiko wazi, hivyo hakuna haja ya kuwafukuza waandishi kwani
niwajibu wao kuchukua habari.
Tanzania Daima
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment