Bukobawadau

MTERA SHOOTING MABINGWA LUKUVI CUP 2014 KATA YA MIGOLI YAIGAGADUA HOME BOYS MBELE YA WAZIRI NKAMIA

Wachezaji  wa  timu ya Mtera wakiendelea  kuumiliki mpira katikafainali ya Lukuvi Cup kata  ya Migoli Mtera

Mabingwa wa Lukuvi Cup timu ya Mtera  wakimiliki mpita
Mchezaji wa  timu ya Home Boys akiwa chini baada ya mchezaji wa  timu ya Mtera kuupiga kichwa  mpira uliokuwa  ukigombewa
Mashabiki  wakifuatilia  mchezo huo
Naibu  waziri Nkamia  akiwa na makombe ya Lukuvi Cup
Uwanja  ukiwa  umezungukwa na mashabiki kabla ya mchezo kuanza
Shangwe  ya ushindi
waziri Nkamia akimkabidhi zawadi  mchezaji  wa  timu ya MTERA
waziri Nkamia akiwa  na  mchezaji  bora wa  timu  ya mtera Bw.mzambia
-
Waziri Nkamia  akimkabidhi kombe  kepteni wa Home Boys

Mashabiki  wakifuatulia  zoezi la zawadi
Na MatukiodaimaBlog
MTERA Shooting yaibuka mabingwa Lukuvi Cup 2014  kwa kata  ya Migoli jimbo la Isimani baada ya kuifunga timu  pinzani ya Home Boys kwa  jumla ya magoli 4-1 katika mchezo wa fainali  ulioshuhudiwa na mgeni rasmi naibu waziri wa habari ,vijana ,utamaduni na michezo Juma Nkamia.

Mchezo  huo  uliochezwa  juzi katika uwanja wa Migoli Mtera uliokuwa  na upinzani  wa hali ya  juu kwa  timu  zote  kutokana na  kushindwa kuonyeshana  ubabe  dakika  90 za  mchezo kwa  timu hizo kutoka  sare ya goli 1-1  kabla ya  kumsaka mshindi kwa  mikwaju ya  penati ambayo  iliiwezesha  timu ya Mtera Shooting  kuigagadua (kuifunga) Home Boys kwa  jumla ya magoli  hayo 4-1 ambayo  yaliiwezesha  kutwaa kombe na kiteta cha pesa  taslim kiasi cha Tsh milioni 1 kutoka kwa  mbunge  wa  jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi ambae ni  waziri wa nchi  ofisi  ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge.

Kbala ya  dakika  90 za mchezo  kumalizika timu ya Mtera Shooting iliweza  kuwanyanyua mashabiki wake baada ya kujipatia goli la kwanza  dakika ya 86 kwa  mkwaju wa  penati goli lililowekwa  nyavuni na  Mtei Mlimbwa huku dakika ya  88  Frank Jackson aliweza  kuisawazishia timu yake ya  Home boys  goli  hilo hivyo timu hizo  kutoka uwanjani  dakika 90 kwa  bila mbabe  kujulikana.

Hali  hiyo iliweza  kupelekea mashabiki  wa kila  timu na  wachezaji  kupigwa na butwaa ya nani  kutwaa kombe  hilo kabla ya mwamuzi  kutumia njia ya matuta kumpata  mshindi ambae  alitokana na ujuzi  wa  kugusa  nyavu  za mwenzake.

Akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu, Naibu Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo, Juma Nkamia,ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, alisema kuwa vijana wengi Tanzania wanapenda michezo japo bado kuna tatizo kubwa kwa viongozi wa michezo hususani walimu wa timu kwa kutokuwa na mafunzo ya ualimu wa timu.

Mapema  katibu  wa mbunge  Lukuvi ,Thom Malenga  alisema kuwa lengo la mbunge Lukuvi  kuanzisha mashindano hayo ni kuweza  kuhamasisha michezo katika  jimbo  hilo na kuwafanya  vijana  kuepukana na matumizi ya madawa ya  kulevya pamoja na mambo mengine ambayo yanaweza  kuwasababishia  kupata maambukizi ya VVU.

Mbali na  hilo alisem akuwa  kupitia michezo  wananchi  wanakuwa pamoja na kuondokana na masuala ya itikadi  vya  vyama wakati  wa  kufanya  shughuli za kimaendeleo.

Pia  alisema mbali ya mashindano hayo ya ngazi ya kata  pia ameanzisha mashindano ya ngazi ya tarafa  ambapo  bingwa atazawadiwa Power tilla kwa  ajili ya kuanzisha vikundi  vya uzalishaji mali katika tarafa.

Waziri Nkamia akizungumza kabla ya kukabidhi  zawadi kwa  mshindi wa mashindano hayo  alisema kuwa uamuzi  uliofanywa na mbunge Lukuvi katika kuanzisha  michezo ni uamuzi wa kupongezwa kwani mbali ya kutekeleza ilani ya CCM katika  michezo bado amewawezesha vijana kupata  fursa ya kuonyesha vipaji vyao ili kupata nafasi ya kuchezea timu kubwa  zaidi .

Hivyo alisema katika  mchezo huo kwa upande  wake amependezwa na kiwango cha mchezo cha mchezaji wa timu ya Mtera pia alisema  kuwa mbunge  Lukuvi ametenga zaidi ya Tsh milioni 30 kwa ajili ya mashindano ya soka katika  jimbo  hilo la Isimani na yeye kama waziri mwenye dhamana  ya michezo amependezwa  zaidi na jitihada  hizo

" Mimi  katika  kuunga mkono  jitihada hizi za Lukuvi  nawaahidi kuwa  nitawasiliana na Lukuvi  ili  mabingwa wakacheze na timu yangu jimboni Kondoa mkoani Dodoma na mchezo mwingine  waje wacheze hapa Mtera hapo vipi ".

Katika mashindano hayo NKamia alimkabidhi  mshindi wa kwanza kombe na fedha taslimu shilingi milioni 1 huku  mshindi wa pili akuikabidhiwa  kombe na shilingi 500,000,mshindi wa tatu akipewa Tsh  250,000 na mchezaji bora  kutoka timu ya Mtera akipewa Tsh 100,000
Next Post Previous Post
Bukobawadau