Bukobawadau

USIKU WA WINDHOEK BUKOBA WAFANA!

 Usiku wa Windhoek ulioandaliwa katika hotel ya Coffee Tree Inn mjini Bukoba Nov 6,2014  ni tukio litakalobaki kwenye kumbukumbu kwa muda mrefu kwa wale wote walioshiriki.
  Lilikuwa ni tukio la kipekee kwa kuwa lilikuwa na madhumuni mchanganyiko yafuatayo:Mosi, kuwakutanisha wana Bukoba kutoka katika fani na taaluma mbali mbali;Pili, kuwapatia wana Bukoba elimu/ufahamu wa kinywaji cha Windhoek na faida zake kwa mtumiaji na mchango wa kinywaji hicho kwa ustawi na maendeleo ya kijamii na ki uchumi; na Tatu, lilikuwa ni jukwaa la wana Bukoba kubadilishana mawazo juu ya fursa za maendeleo ya uchumi na uwekezaji.
 Mgeni Rasmi katika hafla ya usiku wa Windhek ,Mshauri wa Kimataifa wa Kujiitegemea Fr. James Rugemalira wa Mabibo Breweries akiongea na wadau waliofika katika tukio hilo kwa kwa maudhurio mazuri sana.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Vyama Huru vya Wafanyakazi Duniani (ICFTU/AFRO) Mzee Andrew Kailembo kutoka Bruxelles akitoa neno na kumpongeza  kwa dhati  Fr. James Lugemalira.
 Mdau Mkubwa wa kinywaji cha Windhek,Mama Adventina Matungwa ambaye ndiye  Mkurugenzi The Walkgard Transit Hotel -Bukoba
Mwakilishi wa Mabibo Breweries Kanda ya Ziwa Bw. Godfrey Mwangungulu alikuwa ni burudani ya kutosha katika usiku wa Windhoek pale alipoonyesha umahiri wake kwa kuifahamu bidhaa anayoiuza na kuwaelezea wana Bukoba faida lukuki za kunywa Windhoek Lager au Windhoek Draught.
Mwalimu Peace Kabyemela akiteta jambo Meneja wa Bukoba Coop Hotel
Waalikwa wote walikuwa wanakarimiwa kwa vinywaji hivyo isipokuwa kwa wachache wasiotumia. Godfrey, aliuelezea umati uliohudhuria kwa umahiri mkubwa jinsi bia aina ya Windhoek inavyotengenezwa, kwa maana ya viambatishi vinavyotumika na utaratibu mzima unaotumika kuitengeneza bia ya Windhoek na akasema hiyo ndiyo sababu bia hizo Hazina madhara ya mning'inio wa ziada na kukifanya kiwe kinywaji cha kistaarabu na Chenye urafiki na kazi, amani na maendeleo. 
 Waalikwa waliopata fursa ya kuiongelea bia ya Windhoek hususani wale waliokuwa kwenye hafla ya jana yake na wakapata kuionja Windhoek walitoa uthibitisho wa jinsi kinywaji hicho kisivyo na usumbufu wa aina yoyote yaani mning'inio wa ziada wa harufu ya kukera. Mchangiaji mmoja alidiriki kusema kuwa Windhoek ni bia ya wastaarab na matumizi yake ya naweza kuchangia kupunguza uhalifu ukiilinganisha na vinywaji vingine. Na mchangiaji mwingine alisema Windhoek ni kinywaji cha maendeleo. 
 Changamoto iliyojitokeza ni ile ya mabaa mengi kuiuza Windhoek kwa bei ya juu jambo linalowafanya wengi waishie kunywa aina nyingine za bia. Uongozi wa Mabibo Breweries ulikiri kulitambua tatizo hilo  na kusisitiza kuwa wanawasihi wenye mabaa kutumia bei elekezi za rejareja kwani kutokufanya hivyo kunawaumiza watumiaji na kuwazuia wale ambao wangelipenda kuitumia Windhoek.
 Mr&Mrs Ruge Masabala ni Sehemu ya waalikwa.
Kushoto ni  Bi. Sakina Sinda Wakili wa Serikali Mfawidhi - Mkoa wa Kagera Dr. Hamza Mugula, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukoba
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mshauri wa Kimataifa wa Kujiitegemea Fr. James Rugemalira wa Mabibo Breweries ambaye aliwaahukuru wote waliofika kwenye tukio hilo ambalo mahudhurio yake yalikuwa mazuri sana. Fr. James alizungumzia fursa za uwekezaji zilizopo katika mkoa wa Kagera ambazo zinatokana jiografia ya mkoa ndani ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Soko la Pamoja (Common Market). Alisema mkoa wa Kagera ndiyo kwa kipekee unaoziunganisha nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiwa unapakana na Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya ambayo aliita ni Neema ya kipekee kutoka kwa Mwenyezi Mungu. 
Fr. James aliendelea kusema kuwa wana Kagera wanapaswa kujivunia hiyo neema waliyopewa na Mungu lakini akawasihi wasiishie hapo tu bali watambue fursa zinazoletwa na hiyo neema, wajiandae na kufanya Kazi kwa bidii ili kufaidika na hizo fursa. Alifafanua kuwa neema yenyewe ni Soko la bidhaa mbalimbali hususni mazao ya chakula, Matunda na mboga. Alisisitiza kuwa fursa zilizopo ni nyingi kama zilivyokuwa zimeainishwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, katika hafla iliyofanyika jana yake siku ya Jumatano katika hoteli ya Kolping. Fr. James, aliwahimiza wana Kagera kujijengea utaratibu wa kuwa wanafuatilia na kupata taarifa na takwimu mbalimbali kutoka kwenye taasisi za serikali kwani zipo ili wajue na kutambua fursa Ilizopo na wazitumie kujiletea maendeleo ya uchumi binafsi, mkoa na taifa kwa ujumla.

Fr. James aliitumia fursa hiyo kutanabaisha mipango ya uwekezaji ya kampuni ya Mabibo Breweries katika mkoa wa Kagera. Alisema kudhihirisha kwamba wanahubiri wanachokiamini, Mabibo Breweries iko mbioni kuanzisha kiwanda cha kuzalisha bia aina ya Windhoek katika mkoa wa Kagera ili kuweza kunufaika na soko la nchi zinazouzunguka mkoa wa Kagera na hata nchi za Demokrasia ya Kongo na Sudan Kusini.

Fr. James pia alielezea mipango ya Mabibo Breweries kuwekeza kwenye jamii wanayofanyia biashara. Alisema Mabibo Breweries imetambua ukubwa wa tatizo la utambuzi na tiba ya Saratani za aina mbalimbali. Kwa hiyo wameanzisha mpango kwa kushirikiana na wataalam wa Kansa kutoka India ambapo mwezi Septemba walimleta Daktari Bingwa, Prof. Anthony Pais, ambaye alifanya mihadhara kwa madaktari wa hapa nchini na kutembelea maeneo mbalimbali hapa nchini ili kujionea mwenyewe hali halisi ya ukubwa wa tatizo. 

Fr. James alisema kuwa hali ya Kansa ni mbaya sana nchini mwetu na inachukua maisha ya watanzania wenzetu wengi kutokana na kutokuwepo uwezo wa kuitambua mapema hivyo Mara nyingi wagonjwa hutambua wana maradhi ya Kansa ikiwa imefikia viwango vya juu na hivyo kusababisha vifo. 

Kwa kutambua ukubwa wa hilo tatizo, alisema kwamba Mabibo Breweries  watajenga kituo cha kisasa na cha Kimataifa kwa ajili ya ugunduzi na tiba za Kansa mbalimbali. Kituo hicho kitajengwa ndani ya Maniapaa ya Bukoba, kitajlikana kwa jina la RUTAKWA BYERA INTERNATIONAL DREAM TANK CANCER CENTER.
 Fr. James aliongozana na watu mbali mbali ambao alikaa nao meza kuu nao ni mzee Andrew Kailembo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Vyama Huru vya Wafanyakazi Duniani (ICFTU/AFRO), Bw. Yusto Muchuruza, Mkurugenzi Mtendaji wa KADETFU, Bw. Anic Kashasha, mfanyabiashara na Mshauri (Advisor) wa Fr. James Rugemalira, Dr. Hamza Mugula, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Bi. Sakina Sinda, Wakili wa Serikali Mfawidhi - Mkoa wa Kagera, Bibi Adventina Matungwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Walkgard Hotels & Tours,  Dr. Julius Zelithe wa ICAP na Meneja wa Mabobo Breweries Kagera Bw. Rahim Kabyemera ambaye ndiye alikuwa mwenyeji na muandaaji wa shughuli nzima ya jana ambayo pia ilihudhuriwa na idadi nzuri ya wana habari ambao wameahidi kufanya Kazi kwa ushirikiano mkubwa na Mabibo Breweries. 
 Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Mh. Felician Bigambo, Diwani wa Kata ya Bakoba (CUF) kwa miaka 15 ambayo ndiyo nyumbani kwa Fr. James, Bw. Smart Baitani wa COSAD, na Bi Passy Tindi Barongo miongoni mwa waalikwa wengine wengi. Kati ya waliozungumza jana Mh. Bigambo alitia fora kwa kuyatambua matatizo ya Bukoba. Aliitumia nafasi hiyo kumuhakikishia Fr. James na Mabibo Breweries ushirikiano ili kuhakikisha kwamba mipango waliyo nayo inafanikiwa kwa Bukoba inahitaji sana wawekezaji ili kutengeneza ajira kwa vijana ambalo ni tatizo la kitaifa. Kwa ujumla wote waliozungumza jana walionyesha hali ya kusisimka kutokana na mipango yote ya Fr. James na Mabibo Breweries kwa Bukoba.
 Bw. Yusto Muchuruza, Mkurugenzi Mtendaji wa KADETFU akiongelea fursa za uwekezaji.
 Anaonekana Ndugu Edeick Peter Mulima
 Katika pozi anaonekana Rais wa COSAD Tanzani Ndg Smart Baitani
 Dada Paschazia Barongo akitoa mchango wake wa mawazo katika hafla hiyo
Mshauri wa Fr. James, Bw. Anic Kashasha
 Mh. Bigambo alitia fora kwa kuyatambua matatizo ya Bukoba. Aliitumia nafasi hiyo kumuhakikishia Fr. James na Mabibo Breweries ushirikiano ili kuhakikisha kwamba mipango waliyo nayo inafanikiwa
Mh.Felician Bigango  Diwani kata ya Bakoba akiendelea kufunguka juu ya matatizo mbalimbali yanayo yanayoighalimu bukoba.
 Mwendeshaji wa shughuli hii Ndugu Andrew Mutagobwa Kagya
 Mzee Self Mkude
 Bi. Sakina Sinda Wakili wa Serikali Mfawidhi - Mkoa wa Kagera
 Ndg Smart Baitan Mkurugenzi wa COSAD Tanzania
 Ndugu Audax Mtiganzi.
 Dr. Julius Zelithe wa ICAP
 Mwakilishi wa Mabibo Breweries Kanda ya Ziwa Bw. Godfrey Mwangungulu 
Bw. Godfrey Mwangungulu wa Mabibo Breweries katika ubora wake wa kuongelea kinywaji hiki cha Windhoek.
Ndugu Rahym Kabyemela mwakilishi wa Windhoek Bukoba mara baada ya kumpongeza anampongeza Bw. Godfrey Mwangungulu
Mwanahabari Bi Ashura Jumapili
 Mr & Mrs Felix Mulokozi
 Mzee Stanford  pichani katika hali ya usikivu
 BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu  pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
 Wadau katika hili na lile
 Pichani kushoto ni Ndugu Jamal Kalumuna.
 Ikafika muda wa Waalikwa kupata Mulo.
Katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa Ndg Phinias
 Mzee Yusto Muchuruza, Mkurugenzi Mtendaji wa KADETFU
 Sehemu ya wafanyakazi wa New Coffee Tree Hotel wakiendelea kuwajibika
 Huduma ya Chakula ikiendelea.
 Mr. Novat akipata huduma ya Chakula
Sehemu ya wanahabari  waliohudhuria wakipata Msosi
 Dr. Hamza Mugula akipata msosi.
Ndugu Kagya akiendelea kuwajibika kulingana na ratiba
Mzee Mchurusa anamkaribisha kuhitimisha hafla hii Mshauri wa Ki-mataifa wa kujitegemea (International Independent Consultant) Fr. James Rugemalira,wa Mabibo Breweries.
 Fr. James anamalizia kwa kusema kwamba katika mpango wa uwekezaji katika jamii ambayo Mabibo Breweries kwa kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye aliwatbua maadui watatu Mara tu baada ya kupata uhuru wa Tanganyika kuwa ni UJINGA, MARADHI na UMASKINI, Mabibo Breweries imeamua kuanzisha promotion maalum kupitia kinywaji chake murua cha Windhoek kwa ajili ya kuchangisha fedha za ujenzi wa maabara za shule za Sekondari nchi nzima kuitikia wito wa Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. 
 Fr. James alisema promosheni hizo zitaanzia mkoani Kagera na hususan katika Manispaa ya Bukoba. Alielezea kuwa mazungumzo na uongozi wa Maniapaa ya Bukoba yalikuwa tayari yameanza na akasema kuwa kwa vile tayari kuna ushirikiano mzuri wa kikazi na waandishi wa habari hapa Bukoba, basi mipango itakopokuwa tayari umma wote wa Bukoba utajulishwa kupitia vyombo  vya habari
Kulia anaonekana Mr Focas Equalizer mkali katika maswala ya Muziki ni mtu maarufu na hadimu kuonekana ,watu wa vijijini umwiita (Omkama webyombo)
 Mzee Cathbert Basibila akifanya mrejesho..!
 Kwa matukio ya picha zaidi ya 200 tembelea ukurasa wetu wa facebook kupitia hapa>Bukobawadau Entertainment Media
 BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu  pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241


CREDIT:Anic Kashasha,
P. O. Box 11025,
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.
Mob:+255 754/715-281229
Next Post Previous Post
Bukobawadau