Bukobawadau

VILIO NA HUZUNI VYATAWALA NYUMBANI KWA MAREHEMU MTENSA LEONARD 'KYAKAILABWA'

Tukio la kifo cha ghafla cha Marehemu Mtensa Leonard Pichani kilichotokea tarehe 18 Nov, 2014 majira ya saa nne Usiku maeneo ya Buyekera ndani ya Manispaa ya Bukobaolimewagusa watu wengi kweli Nyota yake imezima duniani na  shughuli ya mazishi yake kufanyika Siku ya Jumamosi Nov 22,Nyumbani kwake Kyakailabwa takribani kilomita 3 nje kidogo ya Mji wa Bukoba.
 Kwanza kabisa familia ya Marehemu Mtensa Leonard inatoa shukrani dhati kwa jinsi ambavyo watu wengi wameguswa na msiba huu na kuonyesha upendo na ushirikiano wa hali ya juu katika kuwafariji, kutoa pole na hata kujitolea kwa hali na mali. Mwenyenzi Mungu aendelee kuwaongezea pale mlipotoa.
 Pili mikakati na maandalizi ya Mazishi ya Marehemu Mtensa Leonard inaendelea vizuri, Bukobawadau Blog tunapenda kuwataarifu kuwa shughuli ya mazishi itafanyika siku ya Jumamosi  Nov 22 majira ya saa 9 alasiri nyumbani kwa Marehemu Kyakailabwa ulipo msiba kwa hivi sasa
 Mama Mzazi wa marehemu Mtensa Leonard akilia kwa uchungu, akilia kwa uchungu.
 Simanzi na majonzi vilitawala msiabani hapo kana anavyo onekana Bi Anitha David Mtensa
 Anaonekana Mama Linna ambaye ni Mjane wa Marehemu Mtensa
 Marehemu Mtensa Leonard tutamkumbuka kwa mengi sana katika nyanja mbalimbali Wema wake upole wake, uwezo wa kuelewena na watu wa rika zote na uwezo Mkubwa sana wa kuzuia hasira zake hakika ni kipaji alichokuwa amepewa na Mwenyezi,
Mama wa Marehemu Mtensa Leonard akilia sana mbele ya Mzee Al Hajj Galiatano.
 Katika hali ya Simanzi Mr Deo Rugaibula Bi Benna mdogo wa Mjane wa Marehemu Mtensa.
 Kijana Godfrey Bwogi wa Club linas.
 Anaonekana Gsmart, Abbas Hussein na Mdau Khakim Kichwabuta.
Mr Emma pichani kushoto na Mdau Yunusu Kambuga
 Wadau wanakutana Kikao cha Charula.
 Kushoto waliokaa ni Mama Lugusha akifuatiwa na Bi Letty pembeni yake ni Mrs Mgisha akiwa amefiwa na Shemeji yake Marehemu Mtensa Leonard
Nani asiemjua Mtensa mtu wa watu asiekuwa na makuu?
 Anawasili msibani hapa Bi Pascazia Barongo
 Mdau Yusuph Abeid Dj Y wa Linas Night Club
 Mama Husna na Mdau Haruna Goronga wakiwa wamefika kuwafariji wafika mapema ya leo
Bi Letty na Mrs Mgisha Bi Teddy
 Mzee Maulid Kambuga pichani kushoto akiwa na Mwenzake Fundi Kambuga kwa jina
Katika hili na lile juu ya kifo cha Marehemu Mtensa Muungwana Mpenda watu,Mzalendo wa kweli!!
Bi Lilian Peter Mwise, Mrs Max AbdulMalik Tungaraza na Mr. Jamal Jamco Kalumuna


 Mdau Gulam Scander Visram na Rahym Kabyemela wakitafakari


Bi Jamila Jamal Kalumuna akiteta jambo na Shemeji yake Ndg Rahym Kabyemela.
 Al hajj Abbakari Galiatano akimfariji na kumpa pole Ndg David Mtensa ,ndugu wa marehemu.
Mr.Gulam Scander Visram na Mzee Deo Rugaibura rafiki wa Marehemu Mtensa Leonard
 Ndugu Innocent Pajero na Ndugu Ruge rafiki wakubwa wa Marehemu Mtensa Leonard
 Ndugu Divo Rugaibula akitoa mkono wa pole kwa Ma Kossi Mama Mzazi wa Marehemu Mtensa Leonard.
 Mr Zully wa Rose cafe , mshikaji , rafiki , swahiba mkubwa wa Marehemu Leonard Mtensa
 Taswira mbalimbali eneo la tukio
 Uncle Majid Kichwabuta akiteta jambo na Mr Deo Rugaibula
 Mr.Sweetbart  pichani

 Bi Asia Kichwabuta pichani
 Uncle Salum na Mama Shemsa Mkude
 Ndugu Divo  na Mzee Richard Ochango
 Super Self Mkude hakika umepata pigo kuondokewa na mtu wako wa karibu mno
 Wadau pichani mara baada ya kuwafariji wafiwa
Taswira mapema ya leo mara baada ya taarifa juu ya msiba huu kuenea.
 Pichani kulia ni Kijana Kelvin Mtensa mtoto wa tatu wa kuzaliwa na Marehemu Mtensa Leonard
Mama Lugusha, Bi Letty, Bi Teddy na Dada Mellency
 Mdau Gulam na Mdau Reymond (Chelsea)
  Haya ndiyo yaliyojiri mapema katika msiba huu mkubwa uliotufika”. ... ambao kwa namna moja ama nyingine walio wengi nje na ndani ya Mkoa  wa Kagera wameguswa na msiba huu”
 Uncle Msafiri pichani kushoto
Wadau mbalimbali wakiwa katika msiba huo
 Mr. Deo Rugaibula akisalimiana na Mzee Galiatano, kulia ni Mzee Maulid Kambuga
Tumuombe Mungu aipokee roho ya marehemu na ampatie pumziko la amani!!!
 Katika hali ya uzuni mkubwa anaonekana Ndugu David Mtensa.
 Anaingia Uncle Thomas ' Katikilo
 Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki kutoka sehemu mbalimbali wako hapa kuonesha ni kiasi gani wameguswa na msiba huu ambao ni simanzi.
 Mr Bube  swahiba mkubwa wa Marehemu Mtensa akiteta jambo na kijana Kelvin Mtensa
Marehemu Mutensa alikuwa ni mpambanaji aliyejitahidi kuibadilisha Bukoba kwa jitihada za ujasitiamali. Ni miongoni mwa wazaliwa wa Bukoba ambao kwao Bukoba ilikuwa ni kila kitu, kuwekeza Bukoba kuna changamoto nyingi. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake litukuzwe.
 Bukobawadau tunatoa pole zetu za dhati kwa familia nzima ya marehemu Ndugu jamaa na marafiki ,Mwenyezi Mungu awape faraja na awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu
Kwa picha zaidi Ingia hapaBukobawadau Entertainment Media


Next Post Previous Post
Bukobawadau