WAZIRI NAGU AZINDUA ZIARA YA WAFANYABIASHARA KUTOKA UBELIGIJI
Mhe. Dr. Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji (wa pili kutoka
kushoto) akijiandaa kuzindua ziara ya Wafanyabiashara kutoka Ubeligiji
iliyoanza leo Dar es salaam. Wa pili kulia ni Balozi wa Tanzania
Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala na wa kwanza kushoto ni Balozi wa
Ubeligiji Tanzania Mhe. Adam Koenraad. Waziri Nagu kazindua ziara hiyo
ya siku saba katika Hoteli ya Serena.