Bukobawadau

ZITTO KAFULILA WASHUTUMIWA SAKATA LA IPTL


SEHEMU YA VIDEO: Maswi akisisitiza Zitto, Kafulila ni washenzi na wala rushwa
SAKATA linalohusu kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), limechukua sura mpya baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kuwashambulia kwa maneno makali, wabunge wawili Zitto Kabwe wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) na David Kafulila wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi). FikraPevu ilikuwapo wakati Maswi akitumia maneno makali kwa kuyarudia, akikejeli nyaraka zinazotajwa kuwa ni ushahidi wa jinsi IPTL ilivyouza hisa zake na fedha kutolewa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika akaunti maalumu ya pamoja (Escrow), akisema nyaraka hizo ni karatasi za kufungia vitumbua zinazosambazwa na wabunge hao aliowaita “washenzi”.
Next Post Previous Post
Bukobawadau