Prof. Anna Tibaijuka akiwa kwenye Press Conference Hyatt Regency Hotel Dar es Salaam leo alhamisi Dec 18, Kulia kwake Ndugu Felix Frances Mulokozi, Mkuu wa Shule ya Kajumulo Girls' High School iliyopo Manispaa ya Bukoba.
SIKU chache kupita baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick
Werema kumwandikia Barua Rais Jakaya Kikwete ya Kujiuzulu na Rais
kuridhia kujuzulu kwake na kumshukuru kwa kazi aliyofanya.
Naye Waziri Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka
amekuja Juu na kuwavaa wanaotaka yeye ajiuzulu na kusema hawezi
kufanya hivyo kutokana na kutohusika katika wizi huo.
Na kusema pesa alizopewa zaidi ya Bilioni 1.6 na Mbia wa Kampuni ya
IPTL bwana James Rugemarila ilikuwa kwa ajili ya kusaidia kuboresha
elimu ya mwanamke na kumkomboa kutoka kwenye hali duni ya elimu.
Kauli hiyo ambayo imekuwa ni Tofauti na Matarajio ya Wengi imetolewa Mda
leo jijini Dar Es Salaam na Waziri huyo wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka wakati wa mkutano na waandishi wa
Habari Pamoja na Mambo Mengine Waziri Tibaijuka akizungumza kwa uchugu
alisema hawezi kujiuzulu kutokana na yeye kutohusika katika ufisadi
huo.
“Mimi Nijiuzulu kwa sababu gani? yaani kwa sababu ya mafanikio
ya kuwakomboa wanawake kwenye Elimu ndio mimi nijuzulu,maana kujiuzulu
kunasababu, na hakuna sababu ya mimi kufanya hivyo na sitofanya hivyo
kwani wanaodai mimi nijiuzulu ni wanafiki wenye nia mbaya na mimi ,na
mimi sijiuzulu ng’o na nikifanya wanavyotaka Rais atashangaa ”alisema
Waziri Tibaijuka.
Waziri Tibaijuka aliongeza kuwa madai anayodaiwa kupewa pesa zaidi
ya Bilioni 1.6 na Mbia wa Kampuni ya IPTL bwana james Rugemalira
ilikuwa kwa ajili ya kuinua elimu ya wanawake kwa kuikomboa shule ya
Barbro Johansoon ambapo waliochangia kwenye Shule hiyo ni wengi kuliko
bwana James Rugemalira.
“Leo natuhumiwa na kila mtu kwamba nimepewa pesa na Rugimalira kwamba ni
za kifisadi,Jamani tuwe wa kweli kuhusu madai haya maana nimepewa pesa
na Rugemalira kwa ajiri ya shule hizi na sio huyo pekee alliyechangia
kwani waliochangia pesa hizi ni watu wengi ikiwema Rais wa Awamu ya
Tatu,Benjamin Mkapa,Mfanya Biashara Maarufu Reginald Mengi na wengine
wengi,inakuwaje leo mchango wa Rugumarila kwa Ajiri ya Elimu kwenye
Shule hii ndio iwe nongwa”
“Kwasababu ukisema ni pesa alizonipa ni za ufisadi wa Escrow sio
kweli,kwani Bodi ya Shule ilimuomba Bwana Rugemalira pesa kwa kutumia
Kampuni yake ya Mabibo Wine na kipindi kile ndio alikuwa kiongozi, sasa
hawa watu wanaozani ni za ufisadi inakuwaje jamani tuwe
wakweli”Aliongeza Waziri Tibaijuka.
Waziri Tibaijuka akiongea kwa uchungu huku kama akitaka kulia
alivishangaa vyombo vya Habari hususani Magazeti kumtuhumu kana kwamba
ndio Mhusika wa Ufisadi wa Escrow
“Taifa la Ujerumani liliteketea kwa Uwongo uliokuwa ukienezwa,na
Tanzania ndio tunaelekea huko yaani Magazeti yananituhumu mimi kwamba
mimi ni mhusika wa Escrow,hivi haya Magazeti yana nini jamani hivi kweli
huyo ni Mwandishi wa Habari kweli,na gazeti linaandika Escrow ya
Tibaijuka,hivi msaada wangu wa kuwakomboa Wanawake kielimu ndio imekuwa
haya jamani mbona hatuna hofu ya Mungu?”alihoji Waziri Tibaijuka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment