Bukobawadau

BALOZI KAMALA AKAGUA HOTELI YA NYOTA TANO PATAKAPO FANYIKA KONGAMANO LA BIASHARA MWAKA 2015

Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala ( wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi ya Afrika Rise ya Ubeligiji baada ya kukagua Hoteli ya Nyota tano ya Chateau Du Lac patakapo fanyika Kongamano la Biashara na Uwekezaji  mwezi Aprili, 2015. Makampuni 500 kutoka Luxembourg, Ufaransa, Canada, Switzerland, Dubai, Ubeligiji, Tanzania, Morocco, DRC na  Algeria yanatarajiwa kushiriki. Tanzania imekaribishwa kushiriki katika Kongamano hilo na itapewa fursa ya kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana Tanzania. Kongamano hilo litafanyika jijini Genval - Ubeligiji.
Next Post Previous Post
Bukobawadau