Bukobawadau

HOTEL YA KISASA 'NALPHIN HOTEL & NIGHT CLUB' KUZINDULIWA RASMI LEO DEC 5,2014

Muonekano wa jengo jipya la NALPHIN HOTEL & NIGHT CLUB lililopo Wilayani Muleba.
hii ni  hoteli mpya yenye ukumbi wa mikutano, harusi na sherehe mbalimbali pia na Ukumbi wa  burudani  wa kisasa kabisa 'Night Club'.
 NALPHIN HOTEL & NIGHT CLUB itazinduliwa rasmi  jioni ya leo Ijumaa Dec 5,2014 na Mgeni rasmi anatalajiwa kuwa Mh.Balozi Khamis Kagasheki ambaye ni Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini.
 Wageni mbalimbali na maarufu ,viongozi na wanasiasa wanatarajiwa kuhudhuria hafla ya Uzinduzi wa hotel hii,Wageni maalum watakao hudhuria ni pamoja na muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba maarufu kama 'Dude' au Yahaya na Msanii wa filamu Elizabeth Michael a.k.a Lulu
 Hii ni hali halisi ya eneo la ndani ya ukumbi harusi na sherehe mbalimbali
 Uzinduzi wa NALPHIN HOTEL & NIGHT CLUB utakwenda sambamba na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kutoka nje na ndani ya mkoa wakisindikizwa na Bendi maarufu ya Mwimbaji nyota wa dansi Muumin Mwinjuma. 
Pia atakuwepo Msanii shilolo ,Mkali huyu  atasimama jukwaani zaidi ya saa nzima akikamua shoo ya ukweli na timu ya wanenguaji wake. kwa usawa zaidi watakuwepo wasanii wachekeshaji(comedians) kutoka kundi maarufu Futuhi 
 Mbele ya macho  ni Mr.&Mrs Nafu ambao ndio wakurugenzi wa Nalphin Hotel &Night-Muleba.
 Salamu za furaha, na pongezi kutoka kwa ndugu na jamaa wa karibu.
 Kwa fahari shangwe na furaha tukiwakatika maandalizi ya mwisho ya Uzinduzi rasmi wa hotel  yetu
Hakika ni full furaha kama inavyo onekana pichani


Moja kwa moja Camera yetu inakutana na  bonge la ukumbi wa Disconi 'Nalphin Night Club' ukumbi umekaa vizuri, Sound ya uwakika ,Taa za kila aina 'Disco Light z' zilizo sambaa kila kona 
Humu ndani kinacho endelea ni maandalizi ya ufunguzi rasmi
 ikiwa ni siku moja kabla
 Aiseee Wadau , hili ni  bonge  la chimbo, jamaa kafanya balaa!!hakika muleba wamepata Kiwanja!
Kwa mtambo yupo The Pro Dj Max,kama anavyo onekana akifinya finya mashine
MPAKA HAPO BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
 Camera yetu uso kwa uso na muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba maarufu kama 'Dude' au Yahaya pichani kulia akishow love na jamaa yake wa karibu Ndugu Fide 'Blonzo Da Öñè'
 Anaingia  Mr. Samson Alfred Makoti maarufu kama 'Tolo'
 Pichani kushoto ni Mratibu wa Shughuli nzima ya Uzinduzi huo  Bi Anitha Zimbihile akifuatia na Mr.Khakimu Kichwabuta mshauri mkuu na mikakati endelevu shughuli ya Uzinduzi wa Nalphin hotel &Night Club iliyopo ndani ya Mji mdogo wa Muleba.
 Miongoni mwa wadau waliofika kuangalia jinsi jengo hilo lilivyo ikiwa ni sehemu ku-appreciate alichofanya Kijana mwenzetu,yupo Mr .Rahym Kabyemela akiwa ameongozana na Kijana Soma B.
 Mr. Rahym Kabyemela kijana mpambanaji  akiteta na Mkurugenzi Nafu na Bi Anitha. 


Kushoto ni Mama Nyimbo decoration,Ni mpambaji anaye zingatia vigezo zaidi kwendana na tukio husika,akitabasamu  pichani na  Eng.Jeremy mtaalam aliye husika na ujenzi wa hoteli hii
Taswira maeneo mbalimbali ndani ya Nalphin Hotel & Night Club
 Bwana Kaka, kama alivokutwa akiwajibika katika mazingira ya 'Nalphin Hotel &Night Club
 Namimi naomba picha...''Hayaaa  kaka jipange"!!
 Muonekano wa  mbele
 Haya na mengineyo  ni Ufunguzi wa Nalphin Hotel iliyopo Muleba.
 Kwa ufupi ni hekaheka za Uzinduzi  tayari wananzengo wanawajibika hii ni amsha amsha!
 Mr. Nafu Mkurugenzi wa Nalphin Hotel &Night Club akimtunza mmoja wa wanenguaji
 Kwa matukio zaidi ya picha ingia hapa>>Bukobawadau Entertainment Media
Mashuhuda juu ya kinacho endelea ikiwa ni siku moja kabla ya Uzinduzi rasmi.
 Hivi ndivo camera yetu ilivyo weza kukuangazia moja kwa moja kutoka pande za Muleba  na kukutana Uso kwa uso na muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba maarufu kama 'Dude' au Yahaya.

 Ikiwa ni amsha amsha ya Ufunguzi wa Ukumbi mpya wa 'NALPHIN HOTEL' Uliopo Wilayani Muleba,Uzinduzi utakao fanyika badae ya leo Ijumaa Dec 5,2014 ,
 Pichani ni Sehemu ya mashuhuda
 Wadau pichani kama walivokutwa na Camera yetu
Mr.Rahym Kabyemela katika picha na Mr Nafu, Mkurugenzi Kijana, asiye na makuu , mpole kwa asili yake  yeye ni mzaliwa wa kijiji jirani cha Kagoma , tunachoweza kusema ndugu tumpongeze
  Muonekano wa ndani ya  Chumba cha kulala wageni
 Muonekano wa ndani ya Vyumba vya kulala wageni.
Pitapita za hapa na pale ,Mgeni rasmi atakuwa Balozi Khamis Kagasheki,wageni maalum ni pamoja na Msanii wa filamu Elizabeth Michael a.k.a Lulu ,Uzinduzi huo utakwenda sambamba na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wakisindikizwa na Bendi ya Victoria Sound chini ya Mwimbaji nyota wa dansi Muumin Mwinjuma.
Msanii shilolo atasimama jukwaani zaidi ya saa nzima akikamua shoo ya ukweli na wanenguaji wake kwa usawa zaidi watakuwepo wachekeshaji wa kundi la Futuhi !!

Katika kuepuka kadhia ya Muhungo jamaaw wamejipanga  vyema hilo ni (Generator) likiwa tayari kwa lolote masaa 24.
 Kwa mbali wadau wakicheck na Camera yetu.
 Tunashuhudia Ng'ombe kadhaa wakiletwa kwa ajili ya maandalizi ya kwa ajili ya kitoweo
Maalum kwa shughuli ya Uzinduzi wa mradi wa hoteli ya kisasa yenye sehemu ya Disco 'Night Club' ukumbi maalum wa mikutano.Ukumbi wa harusi na sherehe mbalimbali.
 Mdau msomaji tunaomba ujiunge na Ukurasa wetu wa facebook kwa kutupia 'like' uweze kupata picha zaidi na habari ninginezo papo hapo kupitia link hii>> Bukobawadau Entertainment Media
 MUHIMU :BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
  EBWANA HEE,NALPHIN HOTEL & NIGHT CLUB NDIO HABARI KUBWA AISEE!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau