Bukobawadau

NENDA AISHA MADINDA


Na Happiness Katabazi
MNENGUAJI wa Muziki wa Dansi nchini ambaye aliwahi kujizolea Umaarufu mkubwa Katika medani za muziki wa dansi Kipindi kile wakati akiwa mcheza show wa Bendi ya African Stars' Twanga Pepeta, Extra Bongo, amefariki Dunia mchana huu.
Nikiwa Kama mwanahabari na Mpenzi wa muziki wa dansi nchini,nilikuwa nikiudhuria maonyesho ya bendi ya Twanga Pepeta Kwani imekuwa ni bendi inayotoa burudani nzuri na Marehemu Aisha alilitumikia kwa muda mrefu.
Hakuna ubishi Kuwa Aisha alikuwa na mvuto wa aina yake awapo stagini na ataakiwepo nje ya kazi yake hiyo ya unenguaji.Aliweza kuifanya kazi yake ya unenguaji vizuri.Nilikuwa napenda kazi yake.
Kuna Msemo usemao Kuchunga Umaarufu wako usipotee ni kazi sana.Naweza Kusema Aisha Hilo lilimshinda la Kuchunga Umaarufu wake Kwani akiwa Twanga na hata alipoama Twanga, marehemu alikuwa akituhumiwa kufanya matendo ambayo yaliporomosha Umaarufu wake kwa kasi Hali liyosababisha mashabiki wake Wengi kupoteza mapenzi kwake na kuanza kupotea Katika majukwaa ya muziki wa dansi.
Hakika Aisha umetutoka ila familia yake itambue Kuwa umeacha alama ya kukumbukwa Katika tasnia ya unenguaji hapa Tanzania.
Wananguaji chipukizi jifunzeni Mema yaliyofanywa na dada yenu Aisha na Manaa yake msiyaige.Naamini mkifuata moyo wake wa kujituma na kuipenda kazi yake ya unenguaji ,Matafika Mbali.
Ukitazama Video ya Wimbo wa Mtu pesa, msinijadili, Famili Confrict ,Nyimbo zote hizo mali ya bendi ya Twanga Pepeta,tu akubaliana na Mimi Kuwa marehemu Aisha Madinda alikuwa ni mnenguaji mzuri.
Wapenzi wa muziki wa dansi nikiwemo Mimi nimesikitishwa sana na kifo Chako.Pole Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka maana ni miongoni mwa watu waliomlea Aisha Kimziki hadi hapo alipofikia.Pole familia ya marehemu.
Aisha sisi tulikulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi. Mungu ailaze roho yako mahali panapo Stahili.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
Disemba 17 Mwaka 2014.
Next Post Previous Post
Bukobawadau