Bukobawadau

TANZIA:KOCHA MSHINDO MADEGA AFARIKI DUNIA

Kifo cha aliyekuwa mchezaji wa Zamani wa mpira wa miguu ,timu za RTC Kagera na timu ya Mkoa Lweru Eagles ,Mshindo Madega kimetokea usiku wa kuamkia leo Jumanne dec 16,2014 nyumbani Kwake Kashai baada ya kuugua kwa muda mfupi!
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Kocha Mshindo Madega kilichotokea leo (Desemba 16 mwaka huu) mjini Bukoba.
Mbali ya kuwahi kuwa mchezaji katika timu ya RTC Kagera, Kocha Madega aliwahi kufundisha timu za Kagera Stars, Mwadui na kombaini ya Copa Coca-Cola ya Mkoa wa
Kagera.
Mchango wake katika mchezo wa mpira wa miguu tangu akiwa kocha na baadaye kocha utakumbukwa daima.
Tunatoa salama za rambirambi kwa familia ya marehemu, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Kagera (KRFA), Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) Mkoa wa
Kagera na klabu ya Bukoba Veterans na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika
kipindi hiki kigumu cha msiba huo. TFF itawakilishwa kwenye msiba huo na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA).
Next Post Previous Post
Bukobawadau