Bukobawadau

VIVUTIO MBALIMBBALI NA CAMERA YETU DEC 1,2014

 Fukwe nzuri za kuvutia  maeneo ya Kahororo ndani ya Manispaa ya Bukoba,Bukoba imebarikiwa kuwa na fukwe za asili ambazo hazifanani na fukwe nyingine zozote duniani.
Na fukwe hizi zikiendelezwa zinaweza kuwa chanzo muhimu cha mapato Mkoani Kagera
 Fukwe ya Ntoro iliyopo katika eneo la Kata  ya Kahororo ndani ya  Manispaa ya Bukoba ,kwa sasa maeneo haya yameanza kuendelezwa na watu binafsi
Jambo la kusitikisha ni kwamba licha ya mwambao wa ziwa Victoria  kubainika kuwa na fukwe bora  ambazo zinaweza kufungua utalii katika ziwa Victoria kama wenzetu wa nchi jirani ya Uganda kwa  upande wetu hadi sasa bado hakujawa na juhudi za makusudi kuhakikisha kuwa fukwe zilizopo zinaibuliwa na kuwa chanzo cha mapato.
 Wananchi wa mikoa ya Kanda ya ziwa ukiwemo mkoa wa Kagera bado hawajanufaika katika sekta ya utalii. Moja ya sababu kubwa ni kwamba wananchi wengi hawajapata elimu sahihi kuhusu utalii na faida zake.
 Mabanda ya wananchi yaliyojengwa pembezoni mwa fukwe hizi.
Taswira  fukwe za Mayonde na Izigo Wilayani Muleba
 Blogger mzalendo Mc Baraka akionyesha fursa zilizopo kwa kuyapitia  maeneo mbalimbali yanaweza  kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi,hapa ni maeneo ya fukwe za Izigo Muleba
 Taswira tarafa ya Izigo Wilayani Muleba. “Utalii sio lazima wageni wa kutoka nje ya nchi, hata Watanzania tunaweza kuwa ni sehemu mojawapo ya kufanya utalii wa ndani."
 Hilo neno nalo ni kivutio cha barabarani!!! 

Ndugu wadau wasomaji kwa matukio ya picha zaidi ya 200, tafadhari 'like' ukurasa wetu wa facebook na share 'post' Zetu kupitia hapa>>Bukobawadau Entertainment Media
 Share ukurasa wetu wa facebook na rafiki zako ili kuwakaribisha kwa habari na matukio ya papo hapo!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau