Bukobawadau

KATIKA PICHA TUKIO LA UJAMBAZI DARAJANI LEO

Waswahili wanasema siku za mwizi 40,hivi ndivyo Polisi walivyo wafanikiwa kutuliza tukio la Ujambazi maeneo ya darajani Zanzibar.
 Mmmoja watuhumiwa wa ujambazi katika maeneo ya darajani akiwa chini ya ulinzi wa Polisi akiwa katika gari waliokuwa kulitumia kwa ujambazi huo.aina ya Rav4.
Wananchi wakiwa na asira wakiwa katika mtaa wa darajani wa wakishuhudia jeshi la Polisi Zanzibar kuzima jaribio la ujambazi katika maeneo ya darajani makonte, na kuwadhibiti majambazi watatu wakiwa katika harakati za kuvumia katika maeneo hayo kwa kutaka kupora, majambazi wawili wamekamatwa na mmoja kukimbia
Mtuhumiwa wa ujambazi akiwa ndani ya gari ya Polisi baada ya kupata kipigo kutoka kwa Wananchi wenye hasira wakati wakiwa katika harakati za kutaka kukimbia jirani na skuli ya darajani baada ya kutelekeza gari waliokuwa wakiitumia aina ya Noah.
Gari aina ya Noah linalosadikiwa lilitumika katika tukio la ujambazi katika maeneo ya darajani likiwa limetelekezwa baada ya watumiwa hao wakiwa katika harakati za kuwakimbia Askari katika eneo la mbele ya skuli ya darajani
 Wananchi wakishuhudia tukio la kufanyika kwa ujambazi katika maduka ya darajani.
CREDIT : ZANZINEWS.COM


Next Post Previous Post
Bukobawadau