Bukobawadau

MAMBO HAYO TOKA 90'S

 Haya Mambo Huwezi Kuwa Umepitia kama Umezaliwa Baada ya Mwaka 90's...
1. Kupakwa GV kwenye kidonda
2. Kung'olewa jino kwa uzi
3. Ubwabwa kupikwa j2 tu
4. Kidonda kuwekwa unga wa 'rangi mbili' a.k.a tetesakrin
5. Kupamba kadi na pamba sebuleni
6. Ukumbi wa sherehe kupambwa kwa toilet paper
7. Kunyolewa na mkasi
8. Kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga
9. Wavulana Kuvaa Nguo ya ndani aina moja nchi nzima VIP, usiombe ikakatika ukakuta imebana Kifua.

10. Ku rewind kanda kwa peni
11. Nchi nzima Kuangalia Movie ya Commando John, Double Impact, Rambo na Bluce Lee..
12. Watoto Wa Mtaa Mzima Kufahamiana sababu ya kucheza Wote Jioni Kombolela na Kibaba..
13. Kuunguzana na tunda ya Ubuyu baada ya kuisugua chini
14. Kukata ndala, ati ni kifutio
15. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele ndefu
16. Kuweka Vibox box kwenye Shati la shule Mgongoni..
17. Kuweka Shati la Shule "Blue" eti liwe zuri.
18. Ubitoz Ulikuwa ni Kusimamisha Kora Ya Shati.
19.8 Ukiandika Barua kwa Umpendae lazima uchore moyo na Mkuki na lazima upulizie Pafyumu ya "YU".

20. Hata kama Mlikuwa mmegombana January lakini Mtu anakuambia "Utaipata Siku Ya Kufunga Shule".
21.hukiagizwa dukani wanatema mate chini hukikuta yameishakauka fimbo
22.Nywele zipakwe mafuta ya zawadi zanzibar, weka kipande cha mtungi (oruguyo) kwenye moto      bordray nywele kama relaxer vile 
23. Kupamba toilet paper ndani, na kunawa bakuli moja wakati wa msosi hata kama mko mia.
 24. Kuchemsha kandambili ilpoanza kubonyea kwenye kisigino ? 
25.Simu hazikuwepo mawasiliano hadi upige mruzi au urushe jiwe juu ya bati.
26.Viatu vya lesso(kwa madada) na mkanda wa kipepeo, kaptura ya kaki, chachacha, full jeans, baiskeriya phonex swala na helo, vikombe vya chuma aka mandela!. Soda ya DOUBLE COLA.
27. Kupiga simu lazima uende posta alafu uombe riverse call
Je wewe unakumbuka nini?
Next Post Previous Post
Bukobawadau