MCH.NA MWALIMU WA KAHORORO ATANGAZA NIA YA KUWANIA UBUNGE BUKOBA MJINI
Mwalimu Aidan Muganyizi Gerald pichani.
Mjini Bukoba kabla hata kipenga hakijapulizwa tayari
Mchungaji na Mwalimu wa Kahororo High School mapema ameshatangaza nia ya
kuwania kiti cha Ubunge jimbo la Bukoba Mjini kupitia CHADEMA
Jimbo la BUKOBA kama yalivyo majimbo mengine mkoani hapa
tayari limeanza kunyemelewa na watangaza nia kutoka vyama tofauti vya siasa.
Akiongea na Bukobawadau Mwalimu Aidan Muganyizi Gerald
amesema;''Nina Umri wa miaka 29,nia na sababu ya kugombea kwanza ni kurudisha
heshima ya mji wetu katika kuongeza kasi ya kusambaza huduma za kijamii katika
sekta ya Elimu na Uchumi,tumeporomoka katika heshima ya Usomi NCHINI ,nikipata
fursa nitawashawishi wahaya wote Duniani kuwekeza Bukoba katika Viwanda na
Elimu,ninaazimia katika kaulimbiu (Back to Bukoba Movement we are willing, It must
become)'',alisema.