Bukobawadau

NGOMA AFRICA BAND NA JINAMIZI LA BONGO DANSI

 Muziki wa Bongo Dansi unapogeuka mzimu na kuwapeleka puta washabiki !
Pia wanamuziki FFU-Ughaibuni kukosa Usingizi.
 Mashabiki.
Ngoma Africa Band
 Ngoma Ngoma Africa band aka FFU wakiwajibika
 Imebainika kuwa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni almaarufu viumbe wa ajabu Anunnaki Alien,inayoongoza na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja,bendi hiyo imejukuta ipo katika hali ya kukosa usingizi tena baada ya kutakiwa kutumbuiza maomyesho zaidi katika msimu ujao wa joto,watayarishaji wa maonyesho makubwa ya nje barani ulaya wanashinikizwa na washabiki wao lazima waipandishe jukwaani Ngoma Africa Band kutokana na mdundo wao Bongo dansi,maporota hao baada kuweka roho juu na washabiki wao nao wamedhamiria kuwapambanisha washabiki hao na bendi maarufu Ngoma Africa band yenye makao yake nchini ujerumani,habari za uhakika zimetonya kuwa bendi hiyo imekubali kuenda kutumbuiza katika nchi za Latvia na Austria na maonyesho mengine katika msimu wa joto.
habari zimetonya kuwa hali hiyo tabia za washabiki kushinikiza katika maonyesho inaifanya bendi ya Ngoma Africa band kuwa katika mzunguko wa maonyesho makubwa na wanamuziki kukosa muda wa kupumzika.Lakini inasemekana kamanda Ras Makunja na kikosi chake wanauwezo wa aina yake wa kuwamudu washabiki wao waliodata akili na jinamizi la muziki wa dansi wa bongo kule barani ulaya.ffu-ughaibuni pia wanasikika online at www.ngoma-africa.com
Next Post Previous Post
Bukobawadau