Bukobawadau

WEZI WANAFICHWA KWA MGONGO WA MAMA ANNA !

Mama Tibaijuka amegeuzwa kuwa ndiye escrow ili serikali kuonyesha inawawajibisha waliohusika
Ukweli ni kuwa ukiacha suala la maadili ya kikazi na mapungufu ya busara, mama Anna Tibaijuka hajatajwa mahali popote kuhusiana na kashfa ya escrow
Watu watajiuliza kwanini kuna na shangwe na shmara shamra za kumzogoa huyu mama tena kuingilia hata maisha yake binafsi”
Kuna majibu ynayoweza kutoa picha kuhusu shamra hizo
Kitendo cha Rais kumfanya ni escrow kimemuumiza sana huyu mama kisiasa. 

Hata hivyo Rais alichagua mahali laini. Hakumtanguliza Werema, Chenge au Maswi kwasababu anazozijua yeye
Anna Tibaijuka alikorofishana na wajenzi wa magorofa na wale waliovamia viwanja. Tunajua kesi zipo mahakamani tena zikihusisha watu wenye pesa. 
Hawa wasingependa kumuona Tibaijuka akibaki ofisini
Kuna kampeni za Urais.
  Mama Anna Tibaijuka ni mmoja wa watu waliokuwa wanaangaliwa kwa jicho mujarabu.
Si kuwa ni tishio kwa makundi husika, mama Anna ni tishio kwa kundi moja lislotajwa.
Hili ni kundi la Wanawake wanaotaka kupunguza ushindani miongoni mwao ili mtu wao apate nafasi

Haya yote mnayoyaona hayafanywi kwa bahati mbaya, ni makusudi kabisa.
Serikali imefanikiwa kuwaondoa katika tatizo halisi na kuwatupia mzoga ili mshangilie.

Kuna wabaya wa Anna nao wapo busy kutumia nafasi aliyoitoa Rais ili kukidhi haja zao za kisiasa na kijamii
Hatusikii watu wakiongelea Kilaini aliyelamba mshiko, Askofu Nzigilwa aliyelamba mshiko, Jaji Utamwa na Mujunizi waliolamba utamu, Ngeleja na baba lao Chenge aliyelamba sawa na Anna Tibaijuka. Hatumsikii Muhongo, Maswi au Werema.
Hao wameachwa ‘wapunzike’ kwasababu si tishio la namna yoyote.
Leo picha za siku za nyuma zinatolewa kumdhalilisha mama Anna.
Hili si jambo jema na wenye akili wataacha kuogelewa katika bwawa la maji taka kama hizi kampeni tunazoziona.
Kama hatusimami katika ukweli, nafsi zetu hazina haki ya kusuta nafasi za wenzetu
 MDAU WA JF ANASEMA KUWA:Mama Tibaijuka  hana role iliyotajwa katika taarifa.
Yeye ni kama Ngeleja, Kilaini, Chenge, Nzigilwa na wengine waliopata mgao wa Mkombozi na Stanbic
 Ni jambo la kushangaza kuwa escrow imekuwa Tibaijuka. Kama waliopata mgao ni wezi, mbona wengine hatusikii habari zao? 
Hoja kubwa hapa ni kuwa wezi wanafichwa kwa mgongo wa Tibaijuka.
Werema hasemwi na ili hali aslishiriki kabisa.Katibu wa Rais Mbena hasemwi, ili hali aliandika barua ya shinikizo

Na kubwa zaidi mfanyakazi wa Ikulu amepewa milioni 800 na hakuna anayesema hilo.

Picha iliyowekwa kumbe ilikuwa wakati akiwa waziri. Watu wanaigeuza kumdhalilisha Anna.
Tumeona picha za nyumba yake, watu wamefunga macho mahekalu ya pesa hizo hizo za wizi kwingine
Watu wanamsema Tibaijuka, hawaulizi account ya stanbic ina akina nani

Hapa mumetupiwa mfupa mnaghangaika nao, wenye nyama wamekaa kimya,Msiogelee katika bwawa la uchafu. 
Nendeni kwa wezi siyo katafuta mahali pa kutengeneza mwizi. Hamzitendei haki nafsi zenu

Ukweli ni kitu kizuri na utakuweka huru ukisimama nao
 
Next Post Previous Post
Bukobawadau