Kamati ya Bunge ya ardhi maliasili na mazingira imeitaja wizara ya
ardhi kuwa kinara wa urasimu na ukiukwaji wa taratibu na sheria za ardhi
kiiasi cha kuchochea migogoro na uchelweshwaji wa mikataba ya ardhi inayotekelezwa na mashirika na idara za serikali.
Akiongea mara baada kamati hiyo akitembelea eneo la uwekezaji wa
shirika la nyumba NHC Mbezi luguluni jijini Dar es Salaam mwenyekiti
wake Mhe. James Lembeli ametaja mapungufu hayo kuwa ni pamoja na kugawa
ardhi mara mbili, kugawa maeneo ya wazi, hifadhi za mito,barabara,
mabwawa pamoja na kukiuka sheria ya uendelezaji wa ardhi kwa kipindi cha
miaka mitatu na kusababisha watu kuhodhi maeneo makubwa kwa muda mrefu
bila ya kuyaendeleza kinyume cha sheria.
Kwa upande wake
katibu mkuu wizara ya ardhi nyumba na makazi Bw.Alphayo Kidata pamoja na
kukiri mapungufu hayo ameeleza kuchochewa na baadhi ya watendaji katika
halasmashauri, manispaa na wizarani kushindwa kusimamia sheria na
kanuni na kujikuta wakiiweka wizara katika wakati mgumu wa kutatua
migogoro akiahidi kusimamia vyema sheria kwa ufumbuzi zaidi.
Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa eneo la uwekezaji mkurugenzi wa
biashara shirika la nyumba NHC Bw. David Shambwe pamoja na kueleza
kutekeleza miradi ya zaidi ya bilioni 400 kwa wakati mmoja nchini kote
ameeleza uwekezajiwa luguruni kuwa wa kituo kikubwa cha bishara, makazi
na usafirishaji kama hatua yake ya kupanua huduma za jiji kutoka
katikati ya jiji la dar es salaam na hivyo kupunguza msongamano wa
kihuduma.
CREDIT;ITV.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment