Bukobawadau

BREAKING NEWS:MH.JOHN KOMBA AMEFARIKI DUNIA


Habari zilizotufikia hivi punde ni kuwa Kapteni John Komba amefariki dunia katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam.
Mpaka kufa kwake Kapteni John Komba alikuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmasauri Kuu ya CCM Taifa na Kiongozi wa bendi ya TOT.
"Bwana alitoa, Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe"

UPDATES; Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba amefariki Dunia leo saa 10 jioni katika Hosptali ya TMJ Mikocheni. Kwa Mujibu wa mtoto wa Marehemu Bw. Jerry Komba amesema kifo cha marehemu baba yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kuwa sukari ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es salaam. Katibu wa mbunge huyo Bwana Gasper Tumaini amesema kuwa mbunge huyo alikimbizwa katika hospitali ya TMJ ambapo ndipo mauti yamemkuta. Aidha Bwana Gaspaer Tumaini ameongeza kuwa mwili wa marehemu umehamishiwa katika hosptali ya Lugalo jijini Dar es salaam ambapo ratiba ya Mazishi bado haijafahamika.
Next Post Previous Post
Bukobawadau