Bukobawadau

MBUNGE WA KENYA AUAWA MJINI NAIROBI

Watu wakiwa wamekusanyika kwenye tukio baada ya mbunge George Muchai kuuawa na watu waliokuwa na silaha mjini Nairobi. 
Mbunge mmoja nchini Kenya amepigwa risasi na kuuawa Jumamosi asubuhi mjini Nairobi, pamoja na walinzi wake wawili na dereva.
George Muchai wa chama cha Kabete, alikuwa akirejea kutoka kwenye mkutano wa kifamilia wakati watu waliokuwa na silaha walipoishambulia gari yake. Afisa polisi amesema mauaji hayo yanaonekana kuwa ni mtindo wa kuhakikisha wanaua kabisa.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema "ameshtushwa na kusikitishwa na mauaji hayo". Amesema anatarajia kuwa polisi watatumia rasimali zote walizonazo kuhakikisha watu hao waliokuwa na silaha wanakamatwa haraka.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amelaani mauaji ya mbunge huyo, akisema ilikuwa sehemu ya mwenendo wa ghasia za kisiasa na ukosefu wa usalama nchini Kenya. Nchi hiyo ya Afrika Mashariki imekumbwa na wimbi la ghasia zinazohusishwa na wanamgambo wa kiislamu.
Next Post Previous Post
Bukobawadau