Bukobawadau

MLANGIRA BEN KATARUGA ATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA NA AHADI YA KUJENGA BWENI

Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii  ya Ben Expeditions  pichani Mlangira Ben Kataruga ameendelea na Utaratibu wa kusaidia makundi maalum ikiwemo mayatima na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii  ya Ben Expeditions  Mlangira Ben Kataruga akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kutembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha  Nusuru Yatima kilichoko katika  kata ya Kashai manispaa ya Bukoba.
Akiwa kituoni hapo Mlangira Ben Kataruga kama sehemu ya jamii ametoa msaada wa fedha taslimu shilingi 500,000/=(shilingi laki tano) .Na kwa kile anachoamini kuwa watoto ndilo taifa la kesho ameahidi msaada wa kuwajengea Bweni la Wavulana katika kituo hicho cha kulelea watoto yatima cha 'Nusuru Yatima' 
 Mlezi wa Kituo hicho Bi Mariam Mahya maarufu kwa jini la Nurudhiha pichani kushoto akieleza historia fupi ya kituo hicho mpaka kuanzishwa kwake.
Mlangira Ben Kataruga akionyeshwa mazingira ya vyumba  vya wavulana wa kituo hiki na kujionea hali ilivyo ,hapo ndipo Mlangira Ben Kataruga anapatwa na huruma kubwa na mladhimu kuchukua hatua ya Kuwajengea Bweni jingine.
 Kwa kutambua uwepo wetu karibu na jamii inayotuzunguka, na namna tunavyo jaribu kuchochea maendeleo kupitia BUKOBAWADAU ,Blogger Mc Baraka akapewa jukumu la kukabidhi msaada wa fedha hizo.
Blogger Mc Baraka akitoa maelezo mara baada ya kukabidhi msaada wa shilingi laki tano zilizotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii  ya Ben Expeditions.
 Bukobawadau tunatoa shukrani za dhati kwa Mlangira Ben Kataruga pia tunawashauri watu wenye uwezo wa kifedha kujenga tabia ya kuwasaidia watu wenye uhitaji ili kuwapunguzia ukali wa maisha.
Mlezi wa Kituo hiki Bi Mariam Mahya akitoa Dua Maalum  ya Shukrani kwa Mlangira Ben.
 Baada ya kushuhudia changamoto zinazowakabili watoto wa kituo hiki naye Mchungaji Deo pichani tayari amepanga kukitembelea kituo hiki kwa siku ya kesho nasi BUKOBAWADAU tunasema Inshallah tutazidi kutoa ushirikiano.
Ndivyo linavyosomeka  Bango la kituo cha kulelea watoto cha 'Nusura Yatima kilichopo katika kata ya Kashai cha  kinachojihusisha na malezi ya watoto Yatima
Mlangira Ben Kataruga kwa ujumla amekuwa na utaratibu wa kuyapa makundi haya  uzito wake,amekuwa akisaidia sehemu mbalimbali kwa kuchangia  mahitaji muhimu na ya msingi kama ya chakula, malazi, elimu na afya.
Next Post Previous Post
Bukobawadau