Bukobawadau

MUONEKANO WA MJI WA BUKOBA LEO FEB,2015

Matukio ya picha mbalimbali zinazo onyesha Mandhari ya Mji wa Bukoba
  Sehemu ya Mji wa Bukoba unavyo onekana kwa juu usawa wa milima ya Kashura.
Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo Vijijini vya ndani na Mikoani
Hekaheka za watu maeneo ya  stendi kuu mjini Bukoba
 Mapema nakutana na Mh.Bi Sakina Sinda akiwa ametulia mahala ,nampa pole na majukumu ya kazi mheshimiwa kabla ya kumuomba kupata picha ya pamoja
  Napata Ukodak na  Bi Sakina Sinda ambaye ni Wakili wa Serikali mfawidhi Mkoa wa Kagera
 Camera yetu inaendelea kumulika mitaa mbalimbali ndani ya Mji wa Bukoba
 Mwanalibeneke Mc Baraka wa Bukobawadau  hakika anapiga picha kwa ustadi wa hali ya juu!
Ndivyo zinavyo onekana hekaheka za wananchi katikati ya Mji wa Bukoba.
( Round about) mjini  Bukoba, kushoto ni Jengo la ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Hii ni barabara ya Uganda kuelekea Bandari ya Bukoba na Hospitali ya mkoa wa Kagera.
 Pichani kushoto ni Mdau Rugo Kyamani akiteta na Mdau Jamal Kalumuna (Jamco)
 Katika picha ya pamoja Mr Rugo Kyamani na Mdogo wake Mr.Man Mlaki
 Hapa ni uwanja wa ndege, wanandugu wakiwa wameongozana na Jamaa zao  waliofika kwa ajili kuelekea Kijijini Kishanda Muleba kwenye shughuli ya kumaliza Matanga ya Mama yao mzazi Marehemu Verdiana petro kyamani ,pichani kushoto ni Mdau Rwezaula Kamungu wa Kishanda
 Jumapili tulivu ,majira ya jioni tayari jua limezama ghafla anaingia mshikaji wangu wa kitambo pichani ni Mdau John Muhazi kutoka pande za Chicago- Illinois
 Kabla ya kuingia Masikani kwa mwanalibene mitaa yenye ukimya Miembeni , Mdau John Muhazi akiwa kaongozana na Kijana mtaalam Sadru Ally (kulia)wanapata picha ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu
 Wakati wanataka kutoka anaingia Swahiba wake wa siku nyingi pichani (kushoto)ni mpambanaji Al Amin Abdul
 Mwisho wa siku tupo na Mr Kangunguna pichani
 Siku ya leo alfajiri  tulivu yenye wingu kwa mbali na ki-jua cha kishkaji tukiwa Uwanja wa Ndege kuagana na rafiki yetu mtu wa watu Mlangira Ben Kataruga
Kwa furaha  na bashasha anaonekana Ndugu Jamal Kalumuna (Jamco Production) akiagana na  rafiki yake Muungwana asiye na makuu, Mlangira Ben Kataruga pichani kulia.
Mji wa Bukoba ukitambulishwa na mnara wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba
 Mandhari ya mji Bukoba usawa wa ziwa Victoria linaonekana Jengo la Space Beach Motel.

Next Post Previous Post
Bukobawadau