Bukobawadau

IMARISHA SACCOS KIGARAMA YAWAVUTIA WAGENI KUTOKA CAMEROON NA DRC CONGO


MAKANISA mbalimbali ya Kikristo yametakiwa kubuni mipango endelevu ya kuinua uchumi wa waamini wao katika jitihada za kupambana na umaskini,badala ya kukaa tu na kusubiri wokovu wa mbinguni.
Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki(07/03/2015 )na Askofu Isack Batome (pichani ) kutoka nchini Cameroon,ambaye  amechaguliwa kuwa mratibu wa makanisa ya Kilutheri  barani Afrika,katika umoja unaojulikana kama United Evangelical Mission(UEM),mkutano uliofanyika Dayosisi ya Kakazini Magharibi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri,mjini Bukoba,alipokuwa akifanya ziara ya kutembelea chama cha kuweka na kukopa  cha  Imarisha Saccos Kigarama Wilayani Missenyi.

Askofu Batome na ujumbe wa maaskofu na wachungaji  tisa kutoka nchi ya DRC-Congo walitembelea chama hicho kwa lengo la kujifunza  mbinu mbalimbali zinazokiwezesha  kufanya vizuri  sana miongoni mwa Saccos za KKKT na hata kwenye vyombo vingine vya fedha hapa nchini.
Mratibu  wa Saccos hizo katika Dayosisi,Lilian Lwakatare alisema wageni mbalimbali wamekuwa wakiitembelea Saccos hiyo kutokana na mafanikio yake yanayotokana na uwazi,na uongozi ulio thabiti,kiasi kwamba Saccos hiyo Desemba mwaka jana ilipata cheti cha nafasi ya kwanza kwa wadau wa taasisi ya fedha iitwayo SELF.

Wajumbe kutoka DRC Congo walisema vyama vyao vya kuweka na kukopa bado havijawa na nguvu,na kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni wakopaji kushindwa kurudisha mikopo,na hivyo kusababisha makanisa kuwafungia huduma za kiroho,na inaposhindikana kulipa huwapeleka mahakamani ili kukamata mali walizoweka dhamana.

Katibu wa Imarisha Saccos Kigarama ,Elieza Kakiziba,alisema chama hicho kina mtaji wa zaidi ya sh milioni mia tatu,kikiwa kimekopesha zaidi  yash milioni 17,na hivyo kuwawezesha wanachama kujenga nyumba bora ,kugharamia elimu ya watoto wao,kupanua biashara,  kilimo na ufugaji n.k
 Mwenyekiti wa Imarisha Saccos Kigarama,Willifried Muhumula akifungua mazungumzo na viongozi wa dini waliowatembelea
 Aliyesimama ni mchungaji Badesire Baleke kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, aliyekuwa akitafsiri lugha-Kiswahili kwa Kifaransa,na Kifaransa kwa Kiswahili
 Ofisi ya Saccos husika
 Jengo linaloonekana ni kitega uchumi cha mjasiriamali wa kuweka na kukopa katika Saccos hiyo
 NA MUTAYOBA ARBOGAST,BUKOBAWADAU,Missenyi
Next Post Previous Post
Bukobawadau