Bukobawadau

KAMPUNI YA SIMU TANZANIA (TTCL) YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 50 KATIKA SHULE YA MSINGI BUNENA ILIYOPO MANISPAA YA BUKOBA


Kampuni  ya Simu Tanzania (TTCL) Ofisi ya meneja Mkoa wa Kagera leo March 6,2015 imekabidhi msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi Milioni mbili nusu (2.5) katika shule ya Msingi Bunena iliyopo ndani ya Manispaa ya Mji Bukoba
Kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya simu nchini TTCL,Msaada huo wa Madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 2.5 umekabidhiwa na Meneja wa TTCL Mkoa Kagera Bw. Salum Mbaya (kulia)
Mgeni rasmi katika hafla  ya makabidhiano iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Bunene alikuwa DAS wa Mkoa wa Kagera Mh.Ndayamukama pichani kushoto.
 Mwenyekiti wa kamati ya shule Bi Happiness Peter akimkaribisha Meneja wa TTCL Mkoa Kagera Bw. Salum Mbaya kabla ya kuanza rasmi kwa hafla ya kukabidhi msaada wa Madawati  kutoka TTCL ikiwa ni  katika kuitikia wito wa kuchangia  maendeleo ya Elimu ya Mkoa wa Kagera na Taifa kwa ujumla .TTCL ni Kampuni inayotoa huduma  za mawasiliano ya simu za mezani, Mikononi na  Takwimu Data katika jamii, hivyo Basi ni muhimu kwao kuchangia  sehemu ya maendeleo katika jamii.
TTCL inahamini kutoa msaada huu wa Madawati utasaidia  kuboresha ufanisi  wa shule na hatimaye kupata matokeo makubwa sasa katika sekta ya Elimu
 Mh.Felician Bigambo Diwani wa kata ya Bakoba  (kushoto)na Kaimu Afisa Elimu msingi ,Manispaa ya Bukoba Bi Lilian Katundu pichani kulia
 Baadhi  ya wafanyakazi wa TTCL Mkoa wa Kagera
 Mwenyekiti wa kamati ya shule Bi Happiness Peter akitoa utambulisho kwa wageni
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunena  Sr. Anatolia Vicent akitoa hotuba yake mara baadaya kupokea msaada wa madawati kutoka TTCL.

Katika hali ya usikivu wanaonekana sehemu ya wadau walihudhuria hafla hiyo
 Mgeni Rasmi Mr.Ndamukama akizungumza na wadau mara baada ya kupokea msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 2.5 kutoka Kampuni  ya Simu Tanzania (TTCL) , kwa shule ya Msingi Bunena iliyopo ndani ya Manispaa ya Mji Bukoba
 Sehemu ya wafanyakazi wa TTCL Mkoa wa Kagera

Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Bunena Sr.Anatolia (kushoto) na Mh.Felician Bigambo Diwani wa kata ya Bakoba  (CUF)wakifurahia maneno ya Mgeni rasmi
Sehemu ya wafanyakazi wa TTCL.
 Meneja wa TTCL Mkoa Kagera Bw. Salum Mbaya,akitoa hotuba fupi mara baada  ya kukabidhi msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi Milioni mbili nusu (2.5) katika shule ya Msingi Bunena iliyopo ndani ya Manispaa ya Mji Bukoba
 Mmoja waafanyakazi wa Kampuni ya simu nchini TTCL akichukua picha kwa ajili ya kumbukumbu
 Taswira mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
 Mh.Felician Bigambo Diwani wa kata ya Bakoba  (CUF)akitoa shukrani kwa niaba ya wakazi wa maeneo  Kata ya Bakobala ilipo shule ya msingi Bunena
 Anaonekana Mwalimu Jawadu wa Shule ya msingi Bunena pichani kulia
Mh. Ashura Hassani Diwani wa Viti maalum CCM akitoa neno
 Walimu wa shule za msingi Bunena
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi shule ya Msingi Bunena wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 2.5  kutoka Kampuni  ya Simu Tanzania (TTCL) iliyofanyika mapema ya Ijumaa March 6,2015 katika  Viwanja vya shule ya Msingi Bunena Mjini Bukoba
 Taswira wakati wimbo wa taifa ukiendelea

Wanafunzi wakiimba nyimbo mbalimbali  mara baada ya kukabidhiwa madawati na TTCL
Mwalimu wa Michezo akiwaongoza wanafunzi wa shule ya msingi shule ya Msingi Bunena kuimba wimbo wa shukrani wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 2.5  kutoka Kampuni  ya Simu Tanzania (TTCL) iliyofanyika mapema ya Ijumaa March 6,2015 katika  Viwanja vya shule ya Msingi Bunena Mjini Bukoba
Mwanahabari wa TCB Charles Mwibea akiwajibika wakati wa hafla ya makabidhiano. 
 Mc muongozaji wa Shughuli hii Vedasto Christopher
Diwani wa viti maalum,Ashura Hassan(kulia) akimshukuru Meneja wa TTCL Mkoa Kagera Mr. Salum Mbaya pichani (kushoto)
Mgeni Rasmi DAS wa Mkoa wa Kagera Mh.Ndayamukama (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TTCL ,wadau na walimu wawakilishi wa Shule ya Msingi Bunena mara baada ya kupokea msaada wa madawati 50
 Katika picha ya pamoja kutoka kushoto ni Meneja wa TTCL Mkoa Kagera Bw. Salum Mbaya, Mh.Felician Bigambo Diwani wa kata ya Bakoba ,Mh. Ashura Hassani Diwani wa Viti maalum CCM na wa mwisho ni Mwenyekiti wa kamati ya shule Bi Happiness Peter.
Over  Maquis Original ni hamsha hamsha ya Vijana wa shule ya Msingi Bunena ikiwa ni furaha ya kukabidhiwa madawati 
 Wanafunzi  wakiendelea kuimba kwa furaha
 Bango la Shule ya Msingi Bunena
Mara baada ya hafla ya kukabidhi msaada huo.
 Meneja wa TTCL Mkoa Kagera Bw. Salum Mbaya akizungumza na wanahabari
Sehemu ya wanahabari wakibadirishana mawazo.
 Sehemu ya Jengo la Shule ya Msingi Bunena
 Ni mategemeo makubwa kwamba Msaada huu utakuwa chachu kwa Wadau wengine katika Sekta mbalimbali kuweza kuchangia katika sekta ya Elimu na hatimaye kuondoa changamoto zinazoikabili  Sekta ya Elimu Mkoani Kagera.
TTCL inaendelea kushirikiana na Wadau mbalimbali katika kuleta Maendeleo kadri hali ya kifedha Itakavyo ruhusu
BOFYA HAPA >>Bukobawadau Entertainment Media kujiunga katika ukurasa wetu wa facebook  kwa matukio ya picha zaidi,tafadhari 'like' ukurasa huo kwa habari na matukio ya papo hapo!!

Next Post Previous Post
Bukobawadau