Bukobawadau

UTAFITI MIKOA 13 NCHINI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WAONYESHA LOWASSA ANAONGOZA

Utafiti uliofanywa katika mikoa 13 hapa nchini kuelekea katika uchaguzi mkuu umebaini kuwa wananchi wanamhitaji kiongozi ambaye atakuwa na nia thabiti ya kupambana na kudhibiti rushwa na ufisadi,kutengeneza ajira,kuboresha elimu pamoja na  kuwawezesha wananchi kupata huduma za afya bila bugudha huku matokeo ya jumla yakionesha kuwa waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa ndie anayeongoza.
Wakitoa matokeo ya utafiti kuhusu kutambua vigezo na matarajio ya wananchi katika kufanya maamuzi ya kuchagua viongozi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hapa nchini uliofanywa na Positive Thinkers Tanzania nakushirikisha viongozi maarufu wa kisiasa 17 katika mikoa 13,watafiti hao wamesema kero namba moja kwa wananchi ni rushwa na ufisadi na kwamba wanamhitaji kiongozi mwenye uwezo na vigezo vya kupambana na kero hiyo na kwamba watafanya uchaguzi kwa kuangalia uwezo wa kiongozi badala ya itikadi ya vyama vyao.

Aidha wametoa ushauri kwa tume ya taifa ya uchaguzi kutumia teknolojia ya FAST WEB APPLICATIONS SYSTEM kwa kuwa mfumo huo unaruhusu kuona bayana hali halisi ya matokeo ya utafiti mahali popote mtafiti anapoingiza takwimu jambo linaloepusha malalamiko ya wizi wa kura.

Wameongeza kuwa kulingana na kura zilizopigwa kuhusu sifa na vigezo vya rais atakayefaa kigezo cha utendaji kwa vitendo kimechukua nafasi kubwa na kupata kura 1619 sawa na asilimia 49 ya kura zote zilizopigwa na kudhihirisha kuwa rais ajaye lazima awe na sifa au historia ya utendaji kwa vitendo vinavyodhihirika.
Next Post Previous Post
Bukobawadau