Bukobawadau

VINARA CHELSEA WAONDOLEWA;CHELSEA 2-2 PSG (agg 3-3)

Timu ya Chelsea imeondolewa rasmi kwenye mashindano ya ligi ya Mabingwa Ulaya kwa sheria ya bao la Ugenini kufuatia sare ya 2-2  na kumpa nafasi PSG kuungana na Bayern Munich ,Porto na Real Madrid  katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa.
 Mchezaji David Luiz anaipatia timu yake ya PSG bao la kusawazisha mnamo dakika ya 90 ya mchezo Chelsea 1-1 PSG
Mchezaji David Luiz  akishangilia bao la kuisawazishia timu yake, David Luiz  ameomba msamaha kwa mashabiki wake wa zamani Stamford bridge baada ya kuwatokomeza
''Nilikuwa nimeahidi kuwa sitashabikia bao endapo nitafunga dhidi ya Klabu yangu ya zamani lakini nilishindwa kujistiri .Poleni sana!''

 Bao la dakika 114 katika muda wa ziada lililofungwa na Mchezaji wa Thiago Silva ndilo lililopelekea kuzima ndoto za vinara hao wa ligi kuu ya Uingereza Chelsea.
 Mchezaji nyota wa PSG Ibrahimovic anaoneshwa kadi nyekundu
Wachezaji wa Chelsea wakitoka Uwanjani vichwa chini
Next Post Previous Post
Bukobawadau