Bukobawadau

TASWIRA MAZISHI YA MAREHEMU LUTENI KANALI PASCAL S. HAULE (MSTAAFU)


Jeneza lenye mwili wa Marehemu, Luteni Kanali Pascal S. Haule likiwa lemebebwa na askari wa JWTZ  linawasili nyumbani kwake Kiluvya Gogoni kutoka katika hospital Lugalo kwa ajili ya misa maalum iliyofanyika nyumbani kwake na kufuatiawa na shughuli ya mazishi
Marehemu Luteni Kanali Pascal S. Haule enzi za Uhai wake.

Marehemu Lt. Col. Pascal Stephen Haule(mstaafu)  alifariki duniatarehe 10/4/2015 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo na shughuli ya mazishi  imefanyika  nyumbani kwa marehemu Kiluvya Gogoni siku ya jumanne 14/4/2015 na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange

Mkuu wa majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange akisalimiana na Ndugu Joh Lugenge muda mchache kabla ya shughuli ya mazishi Luteni Kanali Mstaafu Pascal S. Haule
 
Sehemu ya familia ya marehemu Luteni Kanali Mstaafu Pascal S. Haule wakiwa katika hali ya huzuni ufuatia kifo cha baba yao mpendwa kilichotoea  tarehe 10/4/2015 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo na Mazishi yakafanyika nyumbani kwa marehemu Kiluvya Gogoni siku ya jumanne 14/4/2015


Kushoto anaoneka Kaka Mkubwa Donna Rugaibula akimpa mkono wa pole Mdogo wake Mlangira Justuce  Lugaibura kufuatia kifo cha Baba Mkwe wake Marehemu Luteni Kanali Mstaafu Pascal S. Haule
 Mama Mjane wa Marehemu Luteni Kanali Mstaafu Pascal S. Haule (katikati) na watoto wake pichani wakishiriki Ibada ya mwisho ya kumuaga mpendwa wao, bukobawadau blog tunamuombea mwenyezi Mumgu ampumishe kwa amani mzee wetu.
   
 Umati wa waombolezaji wakishiriki Misa Ibada ya mazishi Marehemu Luteni Kanali Mstaafu Pascal S. Haule iliyo fanyika nyumbani kwake Kiluvya Gogoni
   
Muonekano wa Wadau wakishiriki Ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu Luteni Kanali Mstaafu Pascal S. Haule
 
Mtoto wa Marehemu,Bi Alice Mke wa Mlangira Justuce akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa mpendwa baba yake.
 
Baba Paroko akiwa eneo la kaburi tayari kuongoza shughuli ya mazishi.
 Askari wa JWTZ wakiwa tayari kwa mazishi ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na kupiga risasi kadhaa hewani.

 Sehemu ya waombolezaji na Mlangira Justuce Rugaibura wakiwa eneo la kaburi tayari kwa kushiriki mazishi ya Marehemu Luteni Kanali Mstaafu Pascal S. Haule

Jeneza lenye mwili wa Marehemu Luteni Kanali Mstaafu Pascal S. Haule likiingizwa kaburini na askari wa JWTZ.
   
Watoto wa Marehemu pichani kutoka kushoto ni Bi Mage Ailine na Dada ya Alice wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao mpendwa
 
Kushoto ni Mjane wa Marehemu akiweka mshumaa kwenye kaburi la Mme wake mpendwa  
Wanaonekana Mr. Blayan na Mr .Walter Haule ambao ni watoto wa kiume wa Marehemu wakiwa katika picha ya kumbukumbu na ndugu wa Kike pamoja na Mama yao mzazi.
   
Picha ya kwanza kushoto ni KijanaDelius Rugaibula, katikati kwa mbali anaonekana Mtoto Grace Justuce Lugaibula ambaye ndiye mjuu mkubwa wa Marehemu Marehemu Luteni Kanali Mstaafu Pascal S. Haule 
  
 Hivi ndivyo ilivyo kuwa safari ya mwisho ya Marehemu Luteni Kanali Mstaafu Pascal S. Haule,Bukobawadau tunamuombea roho yake ipate rehema kwa Mungu!.....Amumzike kwa amani!!
  
BUKOBAWADAU Blog tutatoa pole kwa wote waliofikwa na msiba huu,Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe amen!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau