Bukobawadau

OFISI YA WAZIRI MKUU, YATEMBELEA MAENEO YALIYOPATA MAAFA MTWARA.

 Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa shughuli za Kuratibu Maafa, Brig. Jen,  Mbazi Msuya akikagua maafa yaliyosababishwa na mvua katika kalvati la barabara ya mbae inayounganisha vijiji vya Mbae na Mbawala, Mtwara Mikindani, Aprili 2015.(katikati) ni Mhandisi msaidizi wa Halmashauri hiyo, Is-haka Mpaki.
Sehemu ya Barabara ya Mbae ambayo kalvati lake limebomolewa na mvua, barabara hiyo inaunganisha vijiji vya Mbae na Mbawala, Mtwara Mikindani
 Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jen. Mbazi Msuya akioneshwa na Kiongozi wa Matengenezo wa Kampuni ya kuzalisha umeme M&P mkoani Mtwara, Musa Kongola, eneo lililoathiriwa na mvua karibu na kiwanda hicho kwa kusababisha udongo kushuka zaidi ya mita mia kutoka usawa wa bahari.
 Eneo la nchi kavu ambalo udongo umeshuka zaidi ya mita mia kutoka usawa wa bahari, karibu na bomba la kusafirisha gesi na kiwanda cha kuzalisha umeme  cha M&P   Mnazi bay Msimbati Mkoani Mtwara. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Kuratibu shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya akiwaonesha viongozi wa Kampuni ya Kuzalisha umeme mkoani Mtwara M&P jinsi ya kuzuia udongo usishuke zaidi kutoka usawa wa bahari.

Muonekano wa Alama lilipo bomba la kusafirisha gesi, Kiwanda cha kuzalisha umeme cha M&P na sehemu ya nchi kavu ambayo udongo umeshuka zaidi ya kilomita mia kutoka usawa wa bahari katika eneo la Msimbati Mkoani Mtwara
Next Post Previous Post
Bukobawadau