Bukobawadau

WANAOHUDUMIA WATOTO WASHAURIWA KUTOWASAHAU WAJAWAZITO NA WALEMAVU

MASHIRIKA  na mitandao inayojihusisha na kuhudumia watoto Mkoani Kagera, yametakiwa kutoa umuhimu mkubwa kwa watoto walio tumboni(kuwajali mama wajawazito) na wale wenye umri hadi miaka minane,kwani ni kipindi hicho ambako malezi na makuzi ya motto yanahitajika sana,ili baadaye motto huyo akue kwa afya njema kimwili, kiakili na kimaadili.
Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki(jana)na  Elisa Muhingo ambaye ni Mratibu wa  Mkoa  wa shirika la TECDEN,linalojihusisha na malezi na makuzi ya mtoto wakati akiwasilisha ripoti ya utekelezaji kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa shirika hilo uliofanyika ukubi wa Kolping mjini
Bukoba.

Pichani Mwenyekiti wa TACDEN Mkoa wa Kagera,Issa Seleman akifungua mkutano mkuu
TACDEN  linahudumia watoto katika mikoa 17,na Mkoani Kagera linaishirikisha mitandao 40 kutoka wilaya zote za mkoa huo lengo lake likiwa ni kuiunganisha mitandao hiyo kujadili namna bora ya kuwahudumia watoto.
Muhingo aliwasisitiza pia wajumbe hao kuhakikisha wanapotoa takwimu,na pia kutoa huduma wasiwasahau watoto wenye ulemavu mbalimbali kwani hao wako kwenye mazingira magumu zaidi na kuwa baadhi mya mitandao imekuwa haiwajali watoto hao.

Mkutano huo,pamoja na mambo mengine uliamua kutumia raslimali zilizopo kama kutoa elimu kwa watoto na akina mama wajawazito kujitegemea kwa kilimo cha mbogamboga na ufugaji kuku kwa ajili ya lishe na kuuza,badala ya kutegemea misaada ya fedha tu kutoka kwa wafadhili.
Mkutano ulipitisha mapendekezo kadhaa ili yawasilishwe kwa mkutano mkuu wa Taifa wa TACDEN katika kuifanyia marekebisho kadhaa Katiba yake ili mwisho wa siku mtoto aweze kuhudumiwa kwa  kwa kiwango kikubwa.

 Kushoto ni Mratibu wa TACDEN Mkoa wa Kagera,Elisa Muhingo(kushoto)
Afisa miradi wa  TACDEN Kagera,Mwita Isaya(pichani kushoto)
Na Mutayoba Arbogast,Bukoba
Next Post Previous Post
Bukobawadau