Bukobawadau

YANATOKEA KATIKA MAHUSIANO

Najua ni usiku sasa, wengine wamelala wengine bado kidogo, katika wale tulioko katika mahusiano na tunalala na wapenzi wetu tuko wa aina mbili kwa muda huu, wako ambao muda huu wana tamani usiku usiishe na asubuhi isifike kwa kiu kubwa waliyonayo ya kukumbatiana na wapenzi wao, wapo pia ambao wana tamani sana na kumwomba Mungu aongeze spidi ya masaa asubuhi ifike ghafla ili waondokane mapema na huyo aliye lala naye kitanda kimoja au aliyelala sehemu tofauti ndani ya chumba kimoja na hii ni kutokana na machungu mnayoyapitia kwenye mahusiano yenu. Nina habari njema na ya matumaini kwako usiku huu, bado mnaweza kuliamsha penzi lililosinzia au kulifufua lililo kufa, kama tu mkiamua kwa dhati. Alamsiki
Next Post Previous Post
Bukobawadau