Bukobawadau

MAULID & LUNCH YA AQDI YA LALY ABDULGARD NA BI ZUENA MURSHID @ UHURU PLATFORM

Ni taswira kutoka viwanja hivi ilipofanyika shughuli ya Maulid ya harusi ya Bwana Laly na Mkewe Zuena , ni moja ya shughuli zilizopangiliwa vizuri na imependeza sana.
Bwana harusi Bwana harusi Laly AbulGard Bi Harusi Zuena Murshid Sued katika pozi moja matata!
Maharusi na wapambe wao katika picha maalumu kwa ajili ya kumbukumbu.
  Credit kwake Mama Ashura Kitenge Muandaji wa mavazi ya wapambe wa Maharusi wetu.
 Muda mchache kabla ya kuelekea Ukumbini kwa ajili ya Shughuli ya Maulid.
 Ukumbini unaweza kucheck jinsi wanawake walivyojitanda na kupendeza ...!
 Mama Rubby pichani kushoto,Mama Farida , Mh. Janath Mussa Kayanda na Bi Shukuru
 Muonekano Ukumbini watu walivyo enea.
Uwanja wa Uhuru Mjini Bukoba  ukiwa umefunga  utadhani Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid......!
Maharusi akiwapungia watu mkono wakati akiingia Ukumbini .
 Wanapata Dua na baraka kutoka kwa Kiongozi wetu wa Dini,Sheikh Mustafa Sadiq na wazee mbalimbali
Wanaendelea kusalimiana na Viongozi wa Dini kutoka maeneo mbalimbali waliohudhuria.
 Bwana harusi na mambe wake Bw. Hassan Bashir.
 Pichani yupo Haji Murshid pamoja na  Mh. Balozi  Khamis Kagasheki aka 'swahiba' Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini
 Sehemu ya Viongozi wetu wa Dini .
 Umati Ukumbini.
 Shughuli ikiongozwa na Mc mwenye Uwezo mkubwa Uncle Salum 'Organizer'.
Bwana Bushura, akindwa kujizuia baada ya kuguswa na maneno ya  kadhaa ya aya  Qur'an
 Kinacho endelea ni kisomo cha Qur'an ,tupo na Msomaji wa  mlango wa pili wa Qur'an kutoka Katika familia ya Bibi harusi huko Kamachumu.
 Mama Rubby mama Mzazi wa Bwana harusi nae ananyanyuka.

Hii ni harusi ya aina yake imekuwa na Suprise kibao, mfano hili tukio la Bwana harusi kutoa zawadi kwa Viongozi wa Dini Masheikh kuanzia ngazi ya Mkoa na Wilaya pamoja na Maimamu
 Sheikh kutoka kamachumu anakabidhiwa zawadi ya Keki.
 Imamu wa Msikiti wa Jamia akipokea zawadi yake ya blanket
 Mzee Abdulziad Kashinde anawapongeza maharusi na kuwaombea dua
 Sheikh Haruna Kichwabuta akitoa mkono wa pongezi maharu.
 Ndugu Optaty Henry wakati wa kuwapongeza maharusi.
  Bwana harusi Laly AbdulGard anamkumbatia Ndugu Optaty Henry (Katibu)
 Katika Swagar mbalimbali wanaone nwapambe wa Bwana harusi .
 Pichani anaonekana Haji Abbuba Sued na Sheikh Idrisa wakiwapongeza maharusi
 Baadhi ya ndugu, Jamaa na Marafiki wakiendelea kuwapongeza  maharusi
 Wakati wa kutoa zawadi na kuwapongeza.

Wageni waliojumuika pamoja wakiendelea kuwapongeza maharusi na kuwakabidhi zawadi .

Wakati tukiendelea na matukio haya, Muhimu tuwaombee maharusi wetu ndoa yao idumu.

 Bi Sharifa Karwani pichani mtaalam wa  maswala ya mapishi.
 Chereko chereko za harusi zikiendelea...!
 Kwakweli haruzi imependeza, Imependeza....Imenoga na imefunika
 Katika picha maalum kwa ajili ya kumbukumbu
Sheikh wa Wilaya ya Missenyi akitoa Dua.
Bibi harusi katika pozi na  Matron wake Bi Shaira
 Hakika wamependeza maharusi hawa nawapambe wao (Best man na Matron ) Bw. Hassana na Mwanadada Sheira
 Mdau msomaji tunakuomba endelea kuwa nasi kwa matukio zaidi ya Picha na Video Steel loading..!
 Wageni kutoka Kamachumu, nyumbani kwao na Bi harusi wakipata msosi safi ,Pongezi kwake muandaaji mtaalam wa mapishi Bi Sharifa Karwani make msosi ulikuwa na ladha na kuvutia

'WANASEMA ALHAMDULILLAH'!BAADA YA NIKAAH KUFUNGWA 29 MAY 2015 KIJIJINI KAMACHUMU!

NAAAM ni Ijumaa nyingine MAY 29,2015 Camera yetu inajikita pande za Kamachumu kushuhudia tukio la Nikaah katika shughuli ya Ndoa ya wawili hawa, ni shughuli inayo -Make headline katika ukanda huu ,maeneo ya ziwa Victoria na mikoa ya jirani ni kati Bwana Laly AbdulGard na Bi Zuena Murshid Sued  'Omwana Owahibanga'.
 Alhamdulillah nikaah ishafungwa Bwana harusi Laly AbulGard sasa ni halali wa Bi Harusi Zuena Murshid Sued (pichani kushoto)kinachofuata ni  kupata mtiririko wa matukio ya shughuli nzima na shamrashamra za hapa na pale kupita Site yako inayopendwa na wengi tukimaanisha Bukobawadau Blog
 Bwana harusi wetu katika bonge la tabasamu .
Burudani ya Qaswida.
Upande wa pili wanaonekana Wadogo zake na Bi harusi wetu Bi Zuena Murshed.
Sheikh anatoa nasaha zake kabla ya tukio la ndoa.
 Wanamama katika hali ya usikivu.
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Sheikh Haruna Kichwabuta akitoa nasaha kwa wanandoa na waliyomo kwenye ndoa
Mama Mzazi wa Bwana Harusi, Mama Rubby anaguswa na  maneno ya Sheikh Haruna Kichwabuta
Endelea kuwa nasi kwa matukio zaidi ya picha na Sehemu ya Video...
TAYARI PICHA 200 ZINAPATIKANA KATIKA UKURASA WETU WAFEBOOK KUPITIA LINK HII>>BUKOBAWADAU MEDIA  KUMBUKA KULIKE UKURASA HUO KWA HABARI NA MATUKIO YA PAPO HAPO
Next Post Previous Post
Bukobawadau