Bukobawadau

TAMWA Kuwajengea Uwezo Waandishi Uandishi Habari za Uchaguzi

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo akizungumza na baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri hao.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo akizungumza na baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri hao.Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam. Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam. Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo (kushoto) akizungumza na baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri hao. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo (kushoto) akizungumza na baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri hao.Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam. Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam. Sehemu ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya maofisa wa TAMWA (kushoto) wakichukua taarifa muhimu katika mkutano huo. Baadhi ya maofisa wa TAMWA (kushoto) wakichukua taarifa muhimu katika mkutano huo.Mwandishi wa Habari Mkongwe na Miongoni mwa waanzilishi wa TAMWA, Bi. Edda Sanga (kulia) akiwasilisha mada kwa baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri hao. Mwandishi wa Habari Mkongwe na Miongoni mwa waanzilishi wa TAMWA, Bi. Edda Sanga (kulia) akiwasilisha mada kwa baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri hao.[/caption] CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kimepanga kuwajengea uwezo baadhi ya waandishi wa habari nchini juu ya uandishi wa habari za uchaguzi kujiandaa na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2015. Akizungumza katika mkutano na baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo alisema mafunzo hayo yatawaongezea ujuzi wanahabari juu ya uandishi wa habari za uchaguzi kwa ujumla kwa kuzingatia utoaji wa nafasi kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Alisema kundi la wanawake wanaoshiriki kugombea katika nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi na walemavu wamekuwa wakikosa fursa kwenye vyombo vya habari kujinadi kutokana na mfumo na mazingira ya uchaguzi yalivyo, hivyo kuna haja ya kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kuzipa kipaumbele pia na makundi hayo ambayo huachwa nyuma kwenye mchakato mzima. Kwa upande wake Mwandishi wa Habari Mkongwe na Miongoni mwa waanzilishi wa TAMWA, Bi. Edda Sanga akitoa mada kwa wahariri juu ya umuhimu wa vyombo vya habari kutoa nafasi pia kwa wagombea wanawake watakaojitokeza kugombea katika Uchaguzi Mkuu; alisema hali hiyo itawafanya wagombea hao kujinadi kwa ufasaha kama ilivyo kwa wanaume hivyo kupata nafasi ya kusikika. Alivitaka vyombo vya habari kubadilika na kuandika habari za wagombea kwa kina, kufanya uchambuzi wa kutosha na kutumia takwimu zitakazo leta mvuto kwa wasomaji na hatimaye wao kufanya uamuzi sahihi baada ya kuwaelewa vizuri wagombea wao. "...Binafsi naomba 2015 vyombo vya habari tuoneshe aina tofauti za kuripoti...turipoti habari zetu vizuri, tuandike kwa kuzingatia njinsia zote, tufanye uchambuzi wa kina, tuandike kwa kutoa takwimu zenye mvuto. Tuhakikishe wanawake nao watakaogombea wanapata nafasi sawa na kusikika kwa wapiga kura," alisema Bi. Sanga akizungumza. TAMWA imekubali kuwajengea uwezo baadhi ya waandishi wa habari juu ya uandishi wa habari za uchaguzi kwa kuzingatia makundi mbalimbali hasa ya wanawake na walemavu ili nao waweze kusikika kama ilivyo kwa kundi la wanasiasa wa kiume. Tayari maandalizi yanafanywa kukamilisha zoezi hilo mapema kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza. __________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mhariri Mkuu Thehabari.com Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066/0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com
Next Post Previous Post
Bukobawadau