TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YATOA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KWA MFUMO WA BVR MKOANI KAGERA
Tume ya Taifa ya Uchuguzi (NEC)
leo tarehe 14 Mei, 2015 imeanza semina ya mafunzo ya uboreshaji wa Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura kwa mfumo mpya wa
uandikishaji uitwao “Biometric Voters Registraion (BVR) kwa Maafisa Waandikishaji, Waandikishaji
Wasaidizi na Maafisa Uchaguzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Bukoba
katika mkoa wa Kagera.
Katika ufunguzi wa mafunzo hayo
Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe. John Mongella aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya
Bukoba Mhe. Jackson Msome aliwaasa Maafisa waliotarajiwa kupata mafunzo ya
uandikishaji kwa mfumo mpya wa (BVR) kuzingatia mafunzo ili wakati ukifika
wananchi wanaostahili kuandikishwa waweze kuandikishwa bila matatizo.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Kagera
aliwataka wanasiasa na viongozi wa vyama vya siasa kuwaacha watendaji kufanya
kufanya kazi yao ya uandikishaji bila kuingiliwa wala kubughiwa ili zoezi
liweze kufanikiwa kama inavyotarajiwa na kuwapa wananchi haki yao ya msingi
muda ukifika ili waweze kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao.
Pia Mhe. Mongella alivitaka vyama
vya siasa kuhakikisha vinaweka wawakilishi wao katika vituo vya uandikishaji
ili kuangalia zoezi zima linavyoendeshwa ili kama kutakuwepo nakasoro vyama
hivyo vya siasa viweze kutoa ushauri ni wapi pa kurekebisha wakati zoezi
linaendelea ili kusiwepo na malalamiko mara baada ya zoezi kuisha.
Viongozi wa siasa na Wakurugezi
Watendaji wa Halmashauri na Manispaa ya Bukoba wamesistizwa pia kuhamasisha
wananchi kwa njiaq mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wenye vigezo
wanaandikishwa mara zoezi litakapoanza katika Halmashauri za wilaya ili
kuyafikia malengo yaliyokusudiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Bw. Albert Macha Afisa kutoka
kitengo cha uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura akitoa ufafanuzi juu
ya mfumo wa uandikishaji utakavyoendeshwa alisema kuwa kila Halmashauri tayari
imebainisha jumla ya vituo vitakavyotumika kuandikisha wananchi na kila kata
itatumia siku saba za katika kuandikisha
wananchi na vifaa vitahamishiwa katika kata nyingine.
“Tayari vifaa mbambali vya
uandikishaji wa wananchi kwa mfumo mpya wa kielektroniki wa (BVR) vimewasili
mkoani Kagera zikiwemo BVR zenyewe na fomu mbalimbali zitakazotumika katika
uandikishaji wa wananchi na vimesambazwa katika Halmashauri zote za mkoa wa
Kagera, aidha uandikishaji unatarajia kuanza tarehe 21.05.2015 katika mkoa wa Kagera” Alisema Bw. Macha.