Bukobawadau

UZINDUZI WA HUDUMA MPYA YA MAXMALIPO KWA KUTUMIA SIMU YA KIGANJANI

Mkuu wa kitengo cha Biashara Maxcom Africa Bw. Deogratius Lazari (Katikati) Akifafanua Jambo kwa waandishi wa habari ambao hawapo katika picha wakati wa Uzinduzi wa Mfumo Mpya wa kutoa huduma za Maxmalipo kwa kutumia simu ya kiganjani, wengine katika picha ni  Maasifisa wa Kampuni Kulia msimamizi mauzo na Usambazaji kanda ya mashariki Bwan Bw. Thomas Mwakalembile na Geofrey Mwakamyanda

Maxcom Africa maarufu kama MaxMalipo ni kampuni ya kitanzania iliyoanzishwa mwaka 2010 ambayo imewekeza katika kurahisisha maisha ya Watanzania na Waafrika kwa ujumla kiuchumi na kijamii kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano (ICT Technology).

Ili kufikia malengo na Sera ya Taifa ya kutumia mifumo ya kielekroniki kutoa huduma na pia kuwezesha Watanzania walio wengi kufikiwa na huduma hizi (Financial Inclusion)  na pia  kurahisisha ukusanyaji wa kodi na kuongeza ajira, MaxMalipo imeanzisha huduma  mpya itakayomuwezesha mtanzania kulipa bili zote kwa kutumia simu ya kiganjani  aina ya  Smart phone yenye Mfumo utakaojulikana kama SmartMalipo.

Huduma hii inatarajiwa kutoa ajira kwa watanzania takribani laki mbili (200,000)  nchi nzima kufikia mwaka 2016  na hivyo kuchangia ukuaji wa sekta isiyo rasmi ya ajira na kunyanyua uchumi wa Nchi.  Mfumo huu utaweza kurahisisha ulipaji wa bili mbalimbali Mfano; Umeme (Luku), Ving’amuzi vya Televisheni, Vocha za Mitandao yote, Kulipia Kodi za TRA na Baadae Kufanya Miamala ya Kibenki  inayohusisha Kuweka na Kutoa fedha, huduma ambazo kwa sasa zinalipwa kupitia mashine za MaxMalipo.

Huduma hiyo inapatikana kwenye mfumo wa simu ya kiganjani ambapo mtumiaji atalazimika kuweka  mfumo wa SmartMalipo (Download Smart Wakala Application) kutoka tovuti ya Google play au tovuti ya Maxmalipo kwa  kuandika neno ‘SmartMalipo  au Maxmalipo’. Kisha mtumiaji atapata maelekezo ya  jinsi ya ku-install mfumo huu kwenye simu yake na jinsi ya kutumia. Mfumo huu utamwezesha mtumiaji yeyote kuwa Wakala na kulipia huduma zilizo orodheshwa. Mtumiaji  wa  mfumo huu  atajipatia kamisheni kama alivyo wakala mwingine wa Maxmalipo kwa Huduma atakazofanya. 

Watumiaji wa mfumo huu wa SmartMalipo watatambulika kwa jina la ‘Smart Wakala’ popote walipo na kufanya biashara kupitia simu zao za kiganjani. MaxMalipo imeanzisha huduma hii mpya kwa lengo la kuwawezesha watanzania walio wengi kufikiwa zaidi na  huduma za malipo kwa haraka wakiwemo wafanyabiashara wadogo na wenye mitaji midogo  ambao kwa mazingira yao ni vigumu kuwa na Mashine za Maxmalipo. 

 MaxMalipo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza matatizo ya foleni kwenye malipo ya huduma mbalimbali kama bili za TRA, LUKU, DAWASCO, huduma za kibenki na hata katika mifuko ya Hifadhi ya jamii Mfano PSPF.


Mwisho kampuni ya Maxcom Africa - Maxmalipo inatoa rai kwa watanzania hasa wafanyabiashara  kuchangamkia huduma zinazotolewa na kampuni hii ili kuendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia katika mifumo ya utoaji huduma.
Next Post Previous Post
Bukobawadau