KUHUSU WEMA KUGOMBEA UBUNGE
Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu, Wema Abraham Sepetu jana June
16 kupitia kipindi cha Ala za Roho ya Clouds FM alifunguka kuhusiana na
kuchukua fomu ya ubunge wa viti maalumu mkoani Singida pamoja na ishu
ya kutoka na boyfriend wa msanii Linah.
Akizungumza na Diva Loveness wa Ala za Roho, Wema Sepetu alisema:
”Sasa hivi niko singida kwenye maandalizi ya kuchukua fomu kwasababu nagombea ubunge wa viti maalumu mkoa wa singida, kwa hiyo nimekuja huku kuja katika kuhamasisha vijana wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la kupigia kura.
"Nimekuja kujiandikisha huku kwa sababu mama yangu ni mtu wa singida so nimejiandikisha tayari tukutane 15 tena kuja kuchukua fomu kwasababu fomu zinatoka tarehe 14 mwezi wa saba so inshallah tuombe uzima, kampeni zimeshaanza zile ndogo ndogo nashukuru Mungu naendelea vizuri nahitaji support kwa jamii"
Baada ya Maelezo hayo Diva alimuuliza Wema swali:
“…I Know about kampeni za chini chini ambazo ulikuwa unafanya kwa muda mrefu kwaajili ya kugombea Ubunge na umepiga picha kwa Raqay tayari ukiwa na mavazi ya CCM si ndio kampeni pale iko pale pale au??…”
Majibu Ya Wema Sepetu:
“…. Yes nimefanya so ama nilikuwa nazungumza na mangement yangu ambayo yupo Martin kadinda na pia yuko Petiman ambaye yupo katika suala zima la kampeni yangu.
"Watanzania wajue tu yes nitachukua fomu ya kugombea Ubunge wa viti maalumu ya mkoani Singida and tutaona uko mbele itakavyokuwa kwasababu hiki ni kinyang’anyiro naingia, ni kama vile naingia kwenye mapambano yaani vitaani so kuna kupata na kukosa .
"Sifikiri kukosa kwasababu mtu ukifikiri kukosa unajiweka kwenye negative side sana lakini najua kwa nguvu za watanzania na kwa nguvu za wananchi wa Singida wataweza kuniamini na kunipa kura zao."
Katika mahojiano hayo Diva alimuuliza tena Wema Sepetu kuhusu ishu ya kuwa na mahusiano na boyfriend wa Lina ambapo Wema alijibu:
"Huwezi amini hizo habari si za kweli kwasababu tulikuwa tunafanya project zinakuja ila nimeshangaa kuona kwanini Linah ameenda on air kwenye kipindi na kuzungumza hizo habari kuwa natembea na boyfriend wake naomba watu waelewe kwamba sikweli…”
IFUATAYO NI SEHEMU YA MAONI YA WADAU
1.KUTOKA KWA;Mimi Mwanakijiji
Yote Tisa: Kama watu wanaogombea wako hivi kwanini Wema naye asigombee? Ukikubali kina fulani wagombee basi na kina fulani nao waachwe wagombee. Watanzania wakiwachagua wataishi na uchaguzi huo kwa miaka mitano. Kama ana mashabiki wake katika Bongo Movie na hata nje ya Bongo movie kwanini asigombee?
Nina uhakika kama ingekuwa ni Marehemu Kanumba watu wangeunga mkono tu - na alitangaza nia ya kugombea kwa wanaokumbuka.
Tusimnyanyapae kwa sababu ni mwanamke au ametumia vipaji vyake jinsi alivyotumia. Mbona Sugu aligombea akashinda na hajahukumiwa kwa Bongo Flava yake huko Mbeya bali kwa uwakilishi wake kwa wananchi wa Mbeya. Tumesikia Profesa J, Afande Sale wote wanania ya kugombea lakini sidhani kama wamehukumiwa kwa sababu ya muziki wao kwanini iwe kwa Wema?
Ilimradi anatimiza vigezo vya msingi - Rais wa Tanzania, Miaka 18 na hajawahi kufungwa kwa zaidi ya miezi sita (I think) basi aachwe agombee tu.
Lakini upande wa pili una ukweli pia; yeyote anayetangaza kugombea ajue pia ametoa haki ya wananchi kukosoa, kubeza na hata kutounga mkono kugombea kwake. Ndani raha ya demokrasia; siyo wote wanapaswa kumuunga mkono; haijalishi cheo gani. Ndio maana tupo wengine hatuwaungi mkono kina Lowassa na wengine.
Inawezekana tungependa agombee kwa chama kingine isipokuwa CCM; well, ndio uzuri mwingine wa demokrasia pia. Wengine wa Bongo Flava na Bongo Movie wamegombea nje ya CCM na ni haki yao; na wengine wenye kuamini CCM wagombee vinginevyo tutakuwa taifa lenye mawazo ya aina moja tu kama mashine.
MMM
2 KUTOKA KWA MDAU;Mwasakafyuka Ndwanga Samson
·Maisha yanabadilika sana !
Zamani Muda kama huu hekaheka za vunja Jungu , kila mtaa unatukio lake , kila bar inamkasa wake , kila Guest imejaaa ...watu wema wakizazi hiki hawataki tena upuuzi wa kipuuzi!
Lakini kila kizazi kinaupuuzi wake !Leo nimebaini mambo magumu.
Kizazi cha Nyerere kilidhani Uongozi hasa wa uwakilishi wa watu ni jukumu zito lililohitaji weledi , hadhi , nidhamu na adabu ....
Kizazi cha leo hakitaki mchezo , kila mtu anajiona anaviwango , hadhi, Na ujazo wa kutosha kuwa Rais ! Na kwakua tumewekeza katika mwendeno wa kupingana na tabia za kizazi cha jana leo kila mtu Anadhani anaweza kuwa mbunge ! Kumbuka kazi ya Mbunge ni Kutunga sheria na kuisimamia Serikali.
Nawaletea Mbunge Mtarajiwa viti Maaalumu Pichani Wema Isack Sepetuuuuuu