Bukobawadau

Lembeli aitabiria CCM anguko katika uchaguzi mkuu utakao fanyika Octoba mwaka huu.

Mbunge wa Kahama James Lembeli amesema viongozi wa CCM wasipo badili tabia ya kutembea na viongozi mifukoni na kugawa kadi feki kwa watu wasiyo wanachama wa CCM kwa lengo la kutaka kuwaengua wagombea wanao kubalika na kuweka wao CCM itegemee kupoteza majimbo na kata nyingi katika uchaguzi mkuu ujao kwakuwa watanzania wa leo hawadanganyiki na wajue  kuwa kura inapigwa na watu wengi siyo wana CCM pekee.
Mhe. Jamse Lembeli ametoa kauli katika mkutano wa hadhara wilayani kahama kufuatia malamiko ya wananchi waliwakilisha katika mkutano na kudai kuwa kumekuwepo na baadhi ya viongizi wa CCM wanapita na wagombea na kuwalazimisha wananchi wawapigie kura na kugawa kadi feki kwa watu wasiyo wanachama ili kuwang’oa viongozi wapinga ufisadi.
 
Ndipo ukifika wakati kwa Mhe. James Lembeli kusema wilaya ya kahama imetapakaa kadi feki za CCM na kutoa angalizo kwa viongozi wa CCM kuwa  wasipo badilika watavuna mabuwa kwani watanzania wa sasa siyo wa wakati uliyopita hivyo CCM inapaswa kuwa makini kwani hata hivyo viongozi hawo wamekiuka tamko la makamu mwenyekiti wa CCM taifa mzee PHILIPO MANGULA alilolitoa mkoani dodoma.
 
Katika mkutano huo pia wananchi walipata nafasi ya kueleza kero zao zikiwemo za watendaji kulazimisha wawekezaji kuweka katika maeneo ambayo wananchi hawakuridhia kuyatoa  na baadhi ya wanawake kulalamikia huduma mbovu za afya na rushwa  kwa wajawazito na watoto katika hospitali na vituo vya afya.
ITV
Next Post Previous Post
Bukobawadau