Bukobawadau

LIVE STREAM:January Makamba akiwazungumzia watanzania

JANUARI ATATOA HOTUBA HII BILA YA KUSOMA POPOTE. HOTUBA YOTE IPO KICHWANI.

- Januari anasisitiza kuwa Tanzania MPYA itajengwa na viongozi wenye fikra mpya.
- Januari ahaidi kuwa na mawaziri wasiozidi 18 tu katika baraza lake la mawaziri endapo chama chake kikimpa ridhaa ya kugombea urais kupitia CCM.
-Januari Makamba anaorodhesha ajenda tano kuu atakazo simamia endapo chama chake kitampa ridhaa ya kugombea na hatimae kuunda serikali.
....Januari ahaidi kuwa serikali yake itatoa mikopo maalumu kwa vijana watakaomaliza vyuo vikuu ambao watapata changamoto ya ajila ili na wao waweze kufungua makampuni yao ili waweze kujizalishia kipato.
....Pia amesema katika serikali yake atahakikisha sekta ya nyumba ina mchango wa zaidi ya 25%, wakati sasa hivi ni chini ya 4% ikimaanisha Watanzania wengi hawana makazi. Hivyo katika uongozi wake hilo la makazi atalipa kipaumbele tofauti na ilivyo sasa.
....Uvuvi, serikali yake itaanzisha mifuko maaalumu ya kukopesha wavuvi ili waweze kununua vifaa vya uvuvi ili isaidie kuboresha vipato vya wavuvi na pia kukuza sekta hiyo kwa kasi.
....Serikali yangu itaongeza udahili wa walimu haswa kwa masomo ya sayansi. Pia ameahidi kutatua changamoto za walimu kama vile mishahara yao kuwa duni, kukosa posho na stahiki mbalimbali. Ahaidi serikali yake kutatua kero hizo kwa kukuza na kuboresha maslahi yao.
.... RUSHWA, amesema kuwa kulizungumza na kulipigia kelele tatizo la rushwa sio njia ya kulimaliza tatizo hilo.
....ARDHI, jinsi ya kuondoa migogoro kati ya wakulima na wafugaji. Serikali yake itabainisha kisheria maeneo ya kilimo, mifugo na makazi. Pia amesema wakulima na wafugaji watamiliki maeneo yao kisheria. Atatumia teknolojia mpya ya satellite kutekeleza hayo kupitia kituo maalumu kitachoundwa chini ya serikali yake. Lakini pia kituo hicho kitasaidia pia na mambo ya kiusalama.
....AFYA, kila Mtanzania lazima awe na bima ya afya, kila Mtanzania lazima apate huduma bora ya afya bila ya kujali kipato chake   
LIVE;January Makamba akiwazungumzia watanzania
Next Post Previous Post
Bukobawadau