MKUU WA USALAMA WA TAIFA WA RWANDA AKAMATWA UINGEREZA !
London,Uingereza,
Mkuu wa usalama wa taifa wa nchi ya Rwanda Major Gen.Emanuel Karenzi Karake amekamatwa na wanausalama katika uwanja wa ndege wa Heathrow nchini Uingereza mwishoni mwa wiki iliyopita,kwa kutuhuma za mauaji ya kivita mwaka 1994 na baada ya mwaka huo pia.Major Gen.Karenzi Karake aliwekwa kizuwizini na baadaye kufikishwa katika mahakama ya Westminister,amri ya kukamatwa kwa mkuu huyo wa idara ya ujasusi (NISS) ya Rwanda kunatokana na ombi la mahakama ya nchi ya Spain ambayo imeorodhesha watu wapatao 40 kuhusika na makosa ya kivita nchini Rwanda ,mashataka yalifunguliwa 2008 kufuatia uchunguzi uliofanywa na kikosi cha mahaka ya spain kinachoongozwa na Andreu Melles .

Mkurugenzi
mkuu huyo wa usalama wa taifa wa Rwanda Bw.Karenzi Karake mwenye umri
wa miaka 54 bado yupo kiziwizini na anatagemea kupandishwa Kizimbani
tena siku ya Alhamisi.