Bukobawadau

MWANAHABARI EDSON KAMUKARA AFARIKI DUNIA LEO

Mwandishi wa habari Edson Kamukara (pichani) amefariki dunia leo.Taarifa zilizotufikia zinaarifu kuwa Mwandishi huyo aliyepata kuandikia gazeti la Tanzania Daima na baadae kuhamia Mwanahalisi amefikwa na umauti baada ya kulipukiwa na jiko la gesi nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam.Aidha habari kutoka kwa majirani zinaarifu kuwa Kamukara amerejea kutoka Bukoba, na alijisikia vibaya wakati anaenda dukani kununua dawa akaanguka na majirani kusaidia kumpepea na baade kupelekwa kwake ambako alipumzika hadi alipopata nguvu na kuamua kujiandalia chakula na ndipo ajali hiyo kumfika na kugharimu maisha yake.
BUKOBAWADAU Blog inatoa pole kwa wote waliofikwa na Msiba huo na italeta taarifa kamili hapo baadae.
Next Post Previous Post
Bukobawadau