Bukobawadau

AJALI MBAYA NYANGOYE WATU NA JENEZA LAO ALMANUSURA!!

Watu kadhaa wanusurika kifo baada ya Gari aina ya Scania Semi Trailler yenye nambari T299 BYR kupinduka na kuangukia pikipiki tatu barabarani na waendesha pikipiki hizo kunusurika,Moja kati ya pikipiki hizo ilikuwa imebeba jeneza tupu .
 Tukio hilo limetukia hivi punde katika Mlima ya Nyangoye -Hamugembe uliopo barabara ya Uganda mjini Bukoba
 Muonekano wa Jeneza likiwa kwenye pikipiki baada ya mkasa huo
 Mashuhuda eneo la tukio wakitazama ajali hiyo.
 Ndivyo inavyo onekana hali ya pikipiki iliyokuwa imebeba jeneza tupu
  Pikipiki iliyokuwa na abiria (majina hayakutambulika)ikiwa Chini baada ya kuangukiwa na gari hilo
 Umati wa watu ukiwa umekusanyika,wakitazama ajali iliyotokea maeneo ya Mlima wa Nyangoye
Aahaha, kweli kufa kufaana!jamaa pichani ameonekana akichota OIL iliyokuwa ikimwagika!
 Askari wa usalama barabarani wakiwa eneo la tukio
 Katikati ya barabari ya Uganda eneo la Nyangoye-Hamugembe
 Hekaheka za mashuhuda wakitaka kujua  kama kweli hakuna mtu
Next Post Previous Post
Bukobawadau