HUDUMA YA UPASUAJI WA WATOTO WENYE UGONJWA WA KICHWA KUJAA MAJI NA MGONGO WAZI YAZINDULIWA RASMI MKOANI KAGERA KATIKA HOSPITARI YA RUFAA YA MKOA
Shirika lisilokuwa la serikali la
Friends of Children with Cancer Tanzania (FOCC TZ) lazindua rasmi huduma ya upasuaji
wa watoto wenye ugonjwa wa vichwa kujaa maji na mgongo wazi mkoani Kagera
katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa ambapo
jumla ya watoto arobaini wenye tatizo hilo wanatajiwa kufanyiwa upasuaji kuanzia Julai 25-26, 2015.
Mkurugenzi wa shirika la FOCCTZ
Bw. Walter Miya katika uzinduzi huo alisema kuwa baada ya kutoa matangazo
kupitia redio za jamii mkoani Kagera kwa muda wa siku mbili wameweza kupata
watoto 70 wenye tatizo la vichwa kujaa maji na mgongio wazi kutoka katika
wilaya zote saba za mkao wa Kagera na
nje ya mkoa.
Bw. Walter alisema watoto
walioweza kufikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa msaada wa
shirika lake ni 40 na watoto 30 wameshindwa kufika kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo wazazi kutokuwa na uwezo wa kuwasafirisha watoto hao,
pia changamoto ya wananchi kuwa na imani
potofu ya kuwa watoto hao wamerogwa.
Huduma hiyo inatolewa mkoani Kagera na shirika la Friends of
Children with Cancer Tanzania wakishirikiana na Madaktari wataalam wa upasuaji
huo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando pia kutoka katika kitengo cha
Muhimbili Orthopaedic Instutite (MOI) kilichopo Hospitali ya Rufaa ya Taifa
Muhimbili.
Daktari Gerald D. Mayaya kutoka
idara ya upasuaji Hospitali ya Rufaa
Bugando akielezea chanzo cha tatizo la ugonjwa wa kichwa kujaa maji na mgongo
wazi alisema kuwa ni mishipa ya kusafirisha maji kichwani kuziba na kichwa
huanza kuvimba ambapo kuna watoto huzaliwa na ugonjwa huo pia wengine upatwa na
ugonjwa huo wakiwa tayari wamezaliwa
na watu wazima pia hupatwa na ugojwa
huo.
Lengo la kutoa huduma hiyo katika
hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kagera ni kupunguza gharama kwa wazazi wenye
watoto wenye tatizo hilo badala ya
kwenda Bugando na muhimbili wapate
huduma hiyo karibu na maeneo yao. Pia kutoa ujuzi kwa wataalam wa haspitali ya
Rufaa ya mkoa wa Kagera ili wawe wanatoa huduma hiyo katika hospitali hiyo.
Alisema Mkurugenzi wa shirika la FOCCTZ Bw. Walter.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. John
Mongella baada ya kuzindua huduma hiyo na kutembelea wodi ya watoto wenye
tatizo la vichwa kujaa maji na mgongo wazi alisema amejifunza mambo mengi maana mwanzo alijua kuwa ugonjwa huo kwa watoto huzaliwa nao kumbe hata mara baada
ya kuzaliwa au mtu mzima anaweza kupatwa na ugonjwa huo.
Mhe Mongella alitoa wito elimu
kutolewa kwa wingi ili wananchi waweze kujua kuwa ugonjwa huo unatibika ili
wazazi na walezi waweze kuwaleta watoto wenye tatizo hospitali ili wakatibiwe.
Pia aliwashukuru Shirika la FOCCTZ kwa kuzindua huduma hiyo ambayo aliita
huduma takatifu kwani inaokoa maisha ya watoto walio wengi.
Wito, Mhe. Mongella alitoa wito
kwa wananchi wenye uwezo kuweza kushirikiana na shirika hilo ili kuchagia
huduma hiyo kuokoa maisha ya watoto. Pia
alitoa wito kwa Wanahabari wa mkoa wa Kagera na Tanzania kwaujumla kuelimisha
jamii juu ya tatizo hilo ili liweze kupunguzwa kwa kiasi kikubwa.
Naye
Vaileth John Makula (32) mzazi wa Gib Philimoni kutoka Wilaya ya Karagwe
alilishukuru Shirika la FOCCTZ kuleta huduma hiyo Kagera maana anasema kuwa
mwanae Gib alizaliwa katika hali ya kawaida na baada ya miezi minne tatizo la
kuvimba kichwa lilianza na alimpeleka mtoto wake katika hospitali