Bukobawadau

JK AMTEUA LAUREAN RUGAMBWA BWANAKUNU KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA BOHARI YA MADAWA (MSD)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Laurean Rugambwa Bwanakunu (pichani) kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bohari ya Dawa (MSD).
Taarifa iliyotolewa Dar es salaam=, Jumatatu, Julai 6, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Ndugu Bwanakunu unaanzia Juni 23, mwaka huu, 2015.

Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Bwanakunu alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ariel Glaser Paediatric AIDS Healthcare Initiative.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
6 Julai,2015
Next Post Previous Post
Bukobawadau