Bukobawadau

LIVE;FATILIA YANAYOJIRI DODOMA BUNGENI RAIS KIKWETE AKIVUNJA BUNGE 09/07/2015

Kikwete: Mhe Spika, nashukuru kwa nafasi hii. Hatimaye siku ya kulivunja Bunge imewadia. Nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi ya kulihutubia bunge ili kutimiza wajibu wangu huo wa kikatiba. Lakini shukrani yangu kubwa ni kwako kwa kuliongoza bunge hili kwa uhodari mkubwa.
Hakika wewe ni nahodha makini na jemedari hodari. Wewe ndiye mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huu wa juu kabisa katika muhimili huu wa kutunga sheria. Na umethibitisha ya kuwa 'Wanawake wakipewa, wanaweza'.
Niwashukuru wabunge kwa kushiriki vema shughuli za bunge na mmelitendea haki na kuliletea heshima na hadhi.
Kikwete: Nilipofungua Bunge la tisa, nilisema; 'Tutatelekeza wajibu wetu kwa Ari mpya. Nguvu mpya na Kasi mpya'. Niitaja vipaumbele vya kufanyia kazi na ilipofika awamu ya pili, nikafungua Bunge la 10 kwa "Ari zaidi, Nguvu zaidi na kasi zaidi".
Kikwete: Tumekutana na changamoto nyingi sana kama taifa, ikiwemo dalili za chuki za kidini, lakini kupitia mazungumzo tumeweza kukabiliana na changamoto hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa dini na wengineo.
Kikwete: Wanaozungumza hawagombani na humaliza tofauti zao bila kugombana
Kikwete: Nawashukuru wananchi wote kwa ushindi tulioupata kudumisha Umoja wa Nchi yetu; tahadhari ni muhimu bado.
Kikwete: Kama kura ya Maoni ingefanyika tukapata Katiba Mpya, tungekuwa hatuongelei kero kadhaa
Kikwete: Nawashukuru wabunge kwa kuupitisha Muswada wa Gesi na Mafuta
Kikwete: Mazingira ya Kisiasa visiwani Zanzibar yamekuwa bora kuliko awali kabla ya Muafaka kati ya CCM na CUF
Kikwete: Nchi yetu iko salama, mipaka iko salama. JWTZ imefanya kazi na Jeshi letu limeimarishwa nyanja zote
Kikwete: Jeshi letu lina utayari wa kivita kwa kiwango cha hali ya juu. Weledi umepanda kwa kiwango kikubwa Kikwete: Namaliza kipindi changu kama Amiri Jeshi Mkuu kwa kujiamini, kwamba tupo salama!
Kikwete: Mwaka 2005/2006 kulikuwa na matukio makubwa ya Ujambazi, niliahidi kupambana nao. Tumewadhibiti, hali ni tofauti sasa
Kikwete: Lazima tuendelee kutafuta muarobaini wa ajali za barabarani
Kikwete: Changamoto kubwa iliyopo hadi sasa ni msongamano wa wafungwa magerezani
Kikwete: Serikali imetimiza wajibu wake, Bunge limefanya kazi kubwa!
Kikwete: Iwapo Katiba Pendekezwa itapita, nchi yetu itapata heshima kubwa sana
Kikwete: Tumeimarisha demokrasia, wanasiasa wanaandamana, wanatoka nje ya Bunge.
Kikwete: Habari kubwa nchini kwa sasa ni Uchaguzi Mkuu. Tarehe 25 Oktoba ni siku ya Uchaguzi; maandalizi yanaendelea
Kikwete: Tumefanikiwa sana kutoa Uhuru wa Vyombo vya Habari! Tuna magazeti ya Ijumaa, Uwazi, Sani...
Kikwete: There's no Media Censorship in Tanzania ‪#‎PressFreedom‬
Kikwete: Nasikitika kuwa hatukuweza kupata Sheria ya Haki ya Kupata Habari na Media Services Bill; wenzetu wajao watamalizia!
Kikwete: TAKUKURU imepewa meno ya kudhibiti na kupambana na Rushwa. Ina ofisi kila Mkoa na kila Wilaya
Kikwete: Tumepata mafanikio makubwa, mapato ya Serikali yameongezeka. Bajeti ya Serikali imekuwa mara 5 ya mwaka 2005 ilivyokuwa
Kikwete: Tumepunguza utegemezi wa misaada katika Bajeti toka 42% hadi 8% kwa kusimamia ukusanyaji mapato
Kikwete: Sehemu kubwa ya Fedha za Serikali inaenda ktk Ununuzi wa Huduma; bila usimamizi mzuri wizi hutawala!
Kikwete: Nafurahi kuwa Taarifa za CAG zinapewa uzito mkubwa na hatua huchukuliwa. POAC/PAC imefanya kazi nzuri pia
Kikwete: Pale inapobainika kuna wizi, hatua za haraka kuwajibisha wahusika zinachukuliwa hata bila kusubiri kuwasilishwa Bungeni
Kikwete: Hati zimeongezeka Serikalini tokana na utendaji mzuri wa Ofisi ya CAG. Tuliajiri vijana wenye CPA km 780 hivi na kuwasambaza nchini
Kikwete: Ili shughuli zilizopangwa katika Bajeti ziweze kufanyika, inabidi Hazina itoe fedha kwa wakati
Kikwete: Tumeongeza Majaji wa Mahakama ya Rufani toka 8 hadi 16. Majaji wanawake wameongezeka toka 8 hadi 37!
Kikwete: Tunao majaji wakazi 1,266 na kati yao majaji wanawake ni 534
Kikwete: Mrundikano wa kesi utakuwa historia katika muda mfupi ujao tokana na ongezeko la majaji na mahakimu
Kikwete: Ujenzi wa Mahakama kila Mkoa unaendelea katika Mikoa 9. Tunatenganisha kazi ya Upelelezi na Kushtaki
Kikwete: Nimeamua kuanzisha Mkoa mpya wa Songwe kwa kuugawa Mkoa wa Mbeya. Wilaya za Ubungo, Kigamboni zimeanzishwa
Kikwete: Kila mwaka tumeongeza kima cha chini cha mshahara toka TZS 65,000/= (2006) hadi TZS 300,000/= (2015)
Kikwete: Idadi ya wabunge wanawake imeongezeka toka 62 hadi 127 sasa!
Kikwete: Vyuo vikuu kulikuwa na wanafunzi wa kike 10,000+ mwaka 2005 na sasa wamefikia 78,000+
Kikwete: Pato la Taifa limekua kwa 7%, Tanzania ni miongoni mwa mataifa 20 Duniani yenye uchumi unaokua kwa kasi
Kikwete: IMF wanasema Pato la Tanzania ni kubwa kuliko walivyodhania. Tumebakiza kidogo sana kuingia kwenye Nchi za Pato la Kati
Kikwete: Mauzo yetu nje (export) yameongezeka mara 7; mfumko wa bei si mkubwa
Kikwete: Tulianzisha BRN, tulianza na sekta 6; tukaongeza nyingine 3. Ni mpango wenye manufaa makubwa
Kikwete: Tulianzisha PPP ili kuweza kurahisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi
Kikwete: Tulianzisha PPP ili kuweza kurahisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi
Kikwete: Tanzania inaongoza Afrika Mashariki kwa kuvutia uwekezaji mkubwa
Kikwete: Tumepania kulirudisha jembe kwenye jumba la makumbusho, iwe historia
Kikwete: Sekta ya Kilimo nchini imekua kwa kiwango kinachoridhisha
Kikwete: Sekta ya Viwanda imekua ingawa bado jitihada zinahitajika kufanikisha zaidi
Kikwete: Uvuvi haramu umepungua ingawa haujaisha; mapato toka Sekta ya Uvuvi yameongezeka
Kikwete: Sekta ya Utalii inachangia 25% ya mapato ya fedha za kigeni
Kikwete: Ajira zimeongezeka; tuna tishio kubwa la Ujangili hasa unaohusisha Meno ya Ndovu, tumefanya operesheni kadhaa
Kikwete: Viwanda vimeongezeka toka 15,000+ hadi 51,000+ sasa. Tunategemea ukuaji zaidi. Ujenzi wa Liganga/Mchuchuma unaanza mwezi ujao
Sekta ya Madini ni ya 2 kuingiza fedha za kigeni. Tumefanya marekebisho ya mikataba ili itulinde sisi pia
Kikwete: Bei ya dhahabu ikipanda, sekta ya Madini itakuwa ya kwanza kuingiza fedha za kigeni
Kikwete: Migodi mipya 3 imeanzishwa katika miaka 10 iliyopita. Ajira ktk Sekta ya Madini imeongezeka toka 3,500 hadi 15,000+
Kikwete: Tumetenga maeneo 8 kwa ajili ya wachimbaji wadogo ili wasisumbuliwe. Tumeanzisha mfuko wa kuwakopesha pia

Next Post Previous Post
Bukobawadau