Bukobawadau

CCM BUKOBA YAFANYA MKUTANO WA HADHARA KUWATAMBULISHA WAGOMBEA WA UDIWANI NA UBUNGE

 Sehemu ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) BUKOBA Mjini wakimpokea kwa shangwe Mh.Balozi Khamis Kagasheki wakati akiwasili katika mkutano wa hadhara wa chama hicho wa kuwatambulisha wagombea wa nafasi za Udiwani na Ubunge uliofanyika leo Aug 15 katika Uwanja wa Uhuru.
Balozi Khamis Kagasheki akipokelewa kwa shangwe na wanachama wa Chama cha mapinduzi CCM waliohudhuria mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha wagombea wa nafasi za Udiwani na Ubunge Jimbo la Bukoba Mjini
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakibadilishana mawazo
 Waliokuwa wagombea wa CCM mchakato wa maoni Ubunge, pichani kutoka kushoto ni Mwl. Joseph Katalaiya na  Mzee Philbart Nyerere ,kulia kabisa ni Kada mahiri wa Chama .
 Kada wa Chama cha mapinduzi ,Mama Khadja akiwa katika Mkutano wa hadhara wa CCM Bukoba wa wakutambulisha wagombea walioteuliwa kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.
 Bi Jeanifer Murungi Kichwabuta akifurahia jambo.
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo .
 Wagombea  wa Udiwani pichani kutoka kushoto ni Ndugu Justinian K.Kamugisha wa kata Bakoba, Mzee Udd Idd Miru wa Kata Bilele na Ndg Richard Gasper mgombea kata Miembeni
 Ndugu Smart Petro Baitani ,mgombea Udiwani  Kata ya Kagando mara baada ya kukabidhiwa fomu rasmi kuwa  mshika bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu ngazi ya Udiwani kata  Kagondo
 Mgombea Udiwani kata Miembeni Richard Gasper mara baada ya kukabidhiwa fomu.
Ndugu  Al Masoud Daudi Kalumuna Mgombea Udiwani kata Ijuganyundo mara baada ya kukabidhiwa fomu
 Sehemu ya Wagombea Udiwani watakao peperusha bendera ya CCM,pichani kulia ni Ndugu Sued Kagasheki mgombea wa kata  Rwamishenye
 Mwakilishi wa Mgombea Udiwani kata ya Kashai Ndugu Samora Lyakurwa aliyepata dharula ya safari na kutokuhudhuria mkutano huo,pichani ni Mh.Mwajabu Galiatano
Mbele ya Camera yetu ni wafuasi wa Chama cha mapinduzi
Kitimu timu,Wimbo wa Ccm mbele kwa mbele  ukiwa hewani
 Wadau wakiendelea kufuatilia mkutano huo.
Mmoja wa waigizaji  kundi la uchekeshaji la Futuhi alikuwepo katika mkutano huo
 Balozi Khamis  Kagasheki akiongea katika Mkutano huo,ambapo amewashukuru wana CCM kwa kumchagua tena kuwa mgombea wa jimbo la Bukoba na kuahaidi ushindi wa kishindo.
 Umati mkubwa wa watu ukimshangilia Mh.Balozi Khamis  Kagasheki
 Shangwe za hapa na pale mkutano ukiendelea.
 Sehemu ya wadau pichani wakifuatiliakinachojiri
 Ndugu Hamim Mahmudu Omary ,Katibu mwenezi CCM Mkoa akitolea jambo ufafanuzi
 Mwalimu Mjuni Joseph Katalaiya akitangaza kuvunja kambi
 Katibu wa CCM Mkoa Kagera Ndugu Idd Ali Ame akihutubia Mkutano wa hadhara leo katika Viwanja vya Uhuru Mjini Bukoba
Wananchi waliohudhuria mkutano huo wakiinua mikono kuashiria kumshangilia Katibu wa CCM Mkoa Kagera Ndugu Idd Ali Ame
 Ndugu Obrah Karugira na Ndugu Avith Kato wakifuatilia kwa umakini Mkutano huo.
 Wanaonekana wafuasi wa makada wa CCM mjini Bukoba
 Sehemu ya Wagombea Udiwani, pichani kulia ni Mgombea mwenye Nyota ya kukubalika Ndg Smart Petro Baitani mwenye Shahada ya Uongozi na utawala na uhusiano wa Kimataifa (BA in Public Administration & International Relations ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1998.
 Mwaka 2000-2002 Ndugu Smart Petro Baitani alijiunga na Chuo kikuu cha Metro State,Minnesota na kufuzu shahada ya Uzamili wa Usimamizi wa Biashara ya (MBA-Masters in Business Admistration),aliendelea kusoma Nchini Marekani shahada ya juu ya usimamizi wa Miradi ya kimataifa na Jamii (PMP-Project Management Professional)
 Ndugu Smart Petro Baitani nyota yake ilianza kung'aa pale alipo pata Scholarship ya kwenda nchini marekani mwaka 1998 kwa ajili ya kusomea Shahada ya Sayansi ya Kompyuta na Muziki
Kimkakati zaidi anaonekana Uncle Majid Kichwabuta pichani
Kimkakati eneo la tukio wanaonekana Bwana Jamal Kalumuna na Jumanne Bingwa wanakwamia;“Hatunywi sumu, hatujinyongi, CCM mbele kwa mbele…..tumeipenda wenyewe
Vijana kutoka pande za Kashai wanakwamba CCM ni…chaguo lao milele na wavimbe wapasuke watajijua
 Mwisho BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
Next Post Previous Post
Bukobawadau