Bukobawadau

HONGERA 'RMK' RAMADHANI WA KAMBUGA KWA TUKIO HILI !!

 Mbele ya Camera yetu ni Shabiki mkubwa  na mpenzi wa mtandao wa Bukobawadau,Ndugu Ramadhani Kambuka (RMK) ,akiwa ametulia pembeni ya gari aina ya Toyota Land Cruiser V 8,kitindo kinacho pelekea tumpe hongera yake.
Waswahili wana methali isemayo kwamba, "Mtaka cha uvunguni sharti ainame". Methali hii haitofautiani sana na ile isemayo kuwa; "Mchumia juani hulia kivulini". Katika methali hizi za Kiafrika ndani yake tunapata falsafa ya Kiafrika inayotudhihirishia kwamba, mafanikio yoyote hayaji pasipo kujishughulisha. Hivyo ili mtu yoyote awezekufanikiwa katika ulimwengu huu hanabudi kujishughulisha ipasavyo 
Hongera sana tena sana Baba Karungi kwa  mchuma huu wa thamani kubwa ,Hongera pia kwa mpango huu wa kuweka Jina badala ya namba kwenye gari ,ni mpango tuliozoea kuona kwa Mastaa wageni Mjini kwetu mfano Mlangira Justus Lugaibula 'Baba GRACE na JOJO'
Kinyumbani tunasema; 'Niwe Olimu Omkigo kya Bukoba ' ni wewe tu mjini kwetu Baba Karungi , hakika Upambanaji na kujiongeza ndio habari ya Mjini.
Next Post Previous Post
Bukobawadau