Bukobawadau

MFUTE MACHOZI NEEMA,MPE TABASAMU

Kwa watanzania wengi, hii si habari/stori mpya. Labda cha kukumbusha tu ni kuwa Neema bado yuko hospital ya taifa muhimbili na anahitaji msaada wako.
Neema mwenye miaka 31, mama wa watoto 3, aliyekaa kwenye ndoa ya manyanyaso kwa miaka 15 huko tarime, mwaka jana (2014)mwezi wa tano majira ya sa kumi jioni aliamua kwenda shambani kwake kuchuma mahindi mawili ili akazie njaa huku akiandaa chakula cha jioni (ugali).
Wakati maji ya ugali yakichemka, mume wa Neema alirudi na kumkuta Neema anakula mahindi. Mume alikasirika na kumuuliza Neema ni nani alimpa ruhusa ya kwenda kuvuna mahindi. Neema kwa nia njema akajibu kuwa yeye anajua shamba ni la kwao wote ndio maana alienda kuchuma mahindi hayo ili atulize njaa.
Mume wa Neema alikasirika na kumwagia maji ya moto (ya ugali). Na kuchukua mkono wa Neema na kuudumbukiza jikoni.
Neema aliyekuwa na mimba ya miezi 4 aliungua sana sehemu ya kifua mpaka matiti kunywea, kwenye koo na mikononi.
Ili kuficha ukatili huo mume alimfungia Neema ndani kwa wiki tatu akimuamuru bint yao mwenye umri wa miaka 13 amuhudiwie.

Hali ya Neema ilizidi kuwa mbaya na vidonda kutoka mafunza ndipo bint yao alipoenda kumwambia jirani ambaye alimtorosha Neema na kumpeleka hospitali ya mkoa wa musoma ambapo alikaa hospitali takriban mwaka mmoja kabla ya kuleta muhimbili mwezi wa saba mwaka huu.
Akiwa muhimbili Neema amelazika kukatwa nyama za kwenye paja ili ziungwe kifuani na kwenye koo - kama unavyoona kwenye picha. 
Operation ya mwisho amefanyiwa juzi tar 19.08.2015
Neema hana ndugu wala jamaa, zaidi ya Mkakati Action na wanaharakati wengine.

Wapendwa mama huyu ameteseka kwenye ndoa kwa miaka 15, na anauguza majeraha ya ukatili wa kupindukia kwa mwaka mmoja sasa. Mahindi mawili yametia Neema ulemavu wa kudumu.
Tumfute Neema machozi kwa kuchangia huduma zake za matibabu kupitia namba zake za simu 0656151072 au 0756768305- Neema Mwita Wambura.
Chochote ulichokuwa nacho Neema atakipokea kwa mikono miwili na moyo mkunjufu. sh elfu moja ni bora zaidi ya hakuna. MFUTE NEEMA MACHOZI, MPE TABASAMU
Tafadhali changia ulichonacho leo na tuma ujumbe huu kwa ndugu jamaa na marafiki na katika magroup yote ya whasapp, na mitandao mengine.
Taarifa hii imetolewa na mkakati action kwa niaba ya Neema Mwita Wambura ‪#‎FridayOfAction‬

Next Post Previous Post
Bukobawadau