Bukobawadau

MWANDANI WA RAIS WA BURUNDI AUAWA

Rais Pierre Nkurunziza pichani
Mamlaka nchini Burundi inasema kuwa jenerali Adolphe Nshimirimana ameuawa.
Imeripotiwa kuwa alifariki katika shambulizi la roketi katika gari lake kaskazini mwa mji mkuu wa Bujumbura.
Jenerali Adolphe Nshimirimana alikuwa rafiki wa karibu wa rais Pierre Nkurunziza.
Hata baada ya kuondolewa kama afisa wa idara ya ujasusi mwezi Novemba mwaka jana alikuwa akionekana na wengi kama mwenye ushawishi mkubwa nchini humo.
Alishtumiwa kwa kusimamia oparesheni za kukabiliana na waandamanaji baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza kwamba atawania muhula wa tatu mbali na kuhusika pakubwa katika kuzima jaribio la mapinduzi dhidi ya rais huyo.
Kwa sasa wengi wana hofu ya hatua itakayochukuliwa na wafuasi wa Nshimirimana.
Next Post Previous Post
Bukobawadau