Baadhi ya Wajasiriamali wakiwa katika maonyesho ya bidhaa mbalimbali kwenye kongamano la wajasiriamali lililofanyika Hoteli ya Mbezi Garden mapema mwaka huu. Kongamano la namna hiyo linatarajiwa kufanyika Septemba 26, 2015 jijini Mwanza Ukumbi wa Benki Kuu (BoT), Capripoint.
Na Dotto Mwaibale
WAJASIRIAMALI zaidi
ya 250 wanatarajia kuonyesha bidhaa zao mbalimbali katika kongamano la mafunzo
ya ujasiriamali litakalofanyika jijini Mwanza.
Akizungumza na Dar es Salaam leo, Mratibu wa
kongamano hilo, Getrude Kilyabusebu alisema lengo la kongamano hilo ni kutoa
mafunzo ya ujasiriamali ili kuwajengea uwezo wajasiriamali hao.
"Wajasiriamali hao katika kongamano hilo watapata fursa
ya kuonesha bidhaa zao mbalimbali na pia watapata mafunzo ya jinsi ya kukuza
mitaji yao na mbinu zingine za biashara" alisema Kilyabusebu.
Alisema makongamano ya namna hiyo yamekuwa yakiwasaidia
wajasiriamali hao kujuana na kubadilishana uzoefu wa kibiashara na utengeneza
wa bidhaa zao zikiwemo mbinu za ufugaji na kilimo.
Alisema mafunzo hayo utolewa na wataalamu waliobobea katika
shughuli za ujasiriamali na matunda ya mafunzo ya makongamano hayo yamewanufaisha
wajasiriamali wengi wajasiriamali.
Kilyabusebu alisema kongamano hilo lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania
(Tanzania Business Entrepreneurs Women) lita Septemba 6, 2015 jijini
Mwanza katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT)
Capripoint.
Mratibu huyo alisema kuwa pamoja na mambo mengine kila
mshiriki atalazimika kuchangia gharama kidogo ili kufanikisha kongamano hilo
ambapo katika mafunzo na chakula atatakiwa kulipia sh.30,000, meza ya kuuzia
bidhaa na kuzitangaza sh. 20,000 na mafunzo na meza sh.50,000.
Kilyabusebu alitumia fursa hiyo kuwaomba wajasiriamali wa
kanda ya ziwa kuweza kushiriki katika kongamano hilo ambalo ni muhimu kujifunza
stadi za kazi zao.
Kwa maelezo zaidi kuhusu kongamano hilo unaweza kupiga simu namba 0754032589 /0756334078/0673032589.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
|



ZILIZO TAZAMWA ZAIDI
SIMANZI MAZISHI YA BINTI VANESA PIUS KIJIJINI GERA!
2 Jan, 2023
Vilio Simanzi na huzuni vilitawala wakati wa Mazishi ya Binti Vanesa Kokusimbisa Pius ,Mtoto wa Mwalimu Pius wa Gera wa pili pichani kutoka ...
SHEREHE YA KUFUNGA MWAKA KWA BANDARI KIJIJINI BUGANGUZI
3 Jan, 2023
Kama kawaida kwa kila mwisho wa mwaka Ndugu Frolence Bandari Mishana wa pili kutoka kulia pichani amekuwa na utaratibu wa kuandaa sherehe z...
FAMILIA YA MZEE FREDERICK MUTAFURWA KATIKA IBADA YA KUWAKUMBUKA WAPENDWA WAO
1 Jan, 2023
Askofu Methodius Kilaini,Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Leo Dec31,2022 ameungana na familia ya marehemu Mzee Frederick Mwelind...
IN LOVING MEMORY OF OMULANGIRA JAMES KIKENYA
4 Jan, 2023
Matukio picha Katika Ibada ya Matanga ya Mpendwa wetu Omulangira James Kikenyayu iliyoongozwa na Mhashamu Ask. Method Kilaini, Msimamizi wa...
#PICHA MATANGA YA OMULANGIRA FREDRICK BARUTI- BURUGO MUGEZA
25 Dec, 2022
Ibada ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu tulipoondokewa na mpendwa wetu Omulangira Fredrick Baruti iliyofanya itakuwa December 22,2020 , Nyu...