Bukobawadau

DK MAGUFULI AITEKA IRINGA AWAFAGILIA MWAKALEBELA, MWAMOTO

 Ulinzi ukiwa umeimarishwa wakati msafara wa Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli ukitoka kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa baada ya mkutano wa kampeni kumalizika
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ( wa pili kulia) akiwaongoza wasanii kupiga Push Up  wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Samora, mjini Iringa. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya wasanii wanaomfanyia kampeni nchini kwa kutumia usafiri wa kibabaji  wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Samora, mjini Iringa
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akijinadi kwa Wananchi wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Samora, mjini Iringa
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akmsimamia Mgombea ubunge Jimbo la Kilolo kupitia CCM, Venance Mwamoto akifanya mazoezi ya Push Up wakati wa mkutano wa kampeni mjini Kilolo, Iringa.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mama mkazi wa wa Ifunda akiwa makini kumsikiliza Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni katika Mji wa Ifunda katika Jimbo la Kalenga.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Iringa Vijijini, Shakila Kiwango akitabasamu baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli  katika Mji wa Ifunda, Jimbo la Kalenga.
 Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la KIalenga kupitia CCM,  Mgimwa wakati wa mkutano wa kampeni katika Mji wa Ifunda
 Dk Magufuli akisalimiana na wazee wa kimila wa kabiloa la Wahehe wakati wa mkutano wa kampeni katika Mji wa Ilula Jimbo la Kilolo mkoani Iringa.
 Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Dk Magufuli mjini Ilula
 Dk Magufuli akijinadi wakati wa mkutano wa kampeni mjini Ilula
 Dk Magufuli akipokea kadi za watu waliojiunga na CCM baada ya kuvihama vyama vyao jana mjni Ilula.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Malkia wa muziki wa Taarabu nchini Khadija Kopa akitumbuiza  wakati wa mkutano wa kampeni mjini Iringa
 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, William Lukuvi akitangaza wasifu wa mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja Samora mjini Iringa.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwaeleza wananchi sababu zilizosababisha CCM kutomteua Lowasa kuwa mgombea urais kupitia CCM hasa kutokana na ufisadi wake
 Nap akisisitiza jambo na kuwaomba wananchi kumuombea afya Mgombea urais  kupitia Chadema, Edward Lowassa ili aje ashuhudie CCM ikishashinda urais
 Nape akisalimiana na Dk Magufuli baada kuhutubia na kumpigia kampeni kwenye Uwanja wa Samora, Iringa
 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, Abdalah Bulembo akimwombea kura Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni
 Dk Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mgombea ubunge Jimbo la Iringa, Frederick Mwakalebela wakati wa mkutano wa kampeni mjini Kilolo, Iringa
Dk Magufuli akiwaaga wananchi nje ya Uwanja wa Samora
Next Post Previous Post
Bukobawadau